Advertisements

Thursday, October 23, 2014

Rich Mavoko kunogesha shoo ya Instagram Part Zanzibar

NA ANDREW CHALE
MSANII nyota nchini, Richard Martin maalufu Rich Mavoko anatarajiwa kutumbuiza kwenye shoo kali na ya aina yake ya Instagram Part Zanzibar itayofanyika ndani ya Zanzibar Beach hotel, Novemba Mosi mwaka huu.
Kwa mujibu wa wandaaji wa shoo hiyo kampuni ya Bond Entertainment, kupitia kwa msemaji wa kampuni hiyo Mackson Madoro alieleza kuwa kila kitu kipo sawa kwa ajili ya tukio hilo ambayo mpaka sasa wadau na wapenzi wa burudani wakiwemo wa ndani na nje ya Visiwa hivyo wanaisubiria kwa hamu kubwa.
“Novemba Mosi ambayo itakuwa siku ya Jumamosi, kwa mara ya kwanza, Msanii Rich Mavoko atapiga shoo ya aina yake katika Instagram Part Zanzibar. Hii itakuwa ni kwa mara ya kwanza tokea kwa msanii huyo atoe wimbo wake wa ‘Pacha wangu’ unayotamba kwa sasa” Alisema Madoro.
Kwa upande wake msimamizi wa shoo, Dhamir Ramz Jr alieleza kuwa mbali na msanii huyo kutoa shoo pia kutakuwa na wageni maarufu mbalimbali watakaojumuika kwa pamoja na kupiga piucha kwenye zulia jekundu na watu watakaoudhulia siku hiyo.
“Instagram Part Zanzibar hii si ya kukosa kwani itakuwa na ‘surprise’ za kila aina kutoka kwa watu maarufu watakaopiga picha na wapenzi wa burudani na marafiki watakaojitokeza siku hiyo” alieleza Ramz Jr.
Ramz Jr aliongeza kuwa, shoo hiyo inayotarajiwa kuanzia majira ya mchana mpaka usiku, ni ya watu wote ambapo ulinzi na usalama umezingatiwa kwa kiwango kikubwa na kuwaomba wajitokez kwa wingi huku kiingilio ikiwa ni sh 10,000 kwa kila mmoja.
ambapo pia kutakuwa na zawadi kkutoka kwa wadhamini kwa watu wa mwanzo watakaoingia kwenye siku hiyo ambayo itakuwa ni ya kihistoria kwa kukutana kwa marafiki na kubadilishana mawazo.
Kampuni ya Bond Entertainment, imekuwa ikijihusisha na masuala ya kuendeleza tasnia ya sanaa kupitia muziki na wasanii mbalimbali kupitia kazi zao na kuandaa matamasha kwa wasanii wa ndani na nje.
“This event aims to entertain and bring together users of the social network INSTAGRAM with emphasis to creating a conducive environment for all instagrammers to meet and exchange their ideas in social networking and bring awareness with regards to the power of the social media in providing information first hand in all issues including social, political and economic platforms.
It is only a once in a life time event to meet your fellow instagrammers from diffrent parts of the country. Don't miss it!
The first attendants will be presented with a special gift .. exclusively designed for the event. Be there!!”

No comments: