Barua hiyo ilielekeza malalamiko yake ya moja kwa moja kwa Balozi wa Tanzania Rome Italy Mhe. James Alex Msekela kwamba ameisha toa ahadi ya kupeleka Afisa wa Uhamiaji kushughulikia maswala yao lakini mpaka sasa ni muda mrefu hajamtuma afisa yeyote kwao.
Ndipo Vijimambo ilipoamua kupiga simu Ubalozi huo wa Italy ili kuweza kujua kulikoni na tuliweza kuongea na Afisa Salvatory Mbilinyi (HEAD OF CHANCERY) na tulivyomwelezea walaka tulioupata kutoka kwa mmoja ya Watanzania waishio huko alimpatia mhusika ambaye hakutaja jina lake alijitambulisha kama Afisa Uhamiaji na yeye alikubali uchelewesho wa pasi za kusafiria upo na sababu moja wapo ni mwombaji mwenyewe kuwa na matatizo au faili lake kutokwepo Uhamiaji Makao makuu na sababu nyingine ni ukwasi unaozikumbuka Balozi zetu nchi za nje na kusisitiza hii ndio sababu moja wapo kubwa ya ucheleweshaji huo. Afisa huyo aliongeza kwa kusema kama mwombaji hana tatizo lolote swala lake halichukui muda kutekelezewa japo hakutaja ni muda gani huchukua kama mtu hana tatizo lolote kupata pasi yake. Kuhusu swala la watoto wanaozaliwa huko kukosa kupata pasiport afisa huyo hakuligusia kabisa na kusema yeye sio msemaji wa Ubalozi na kashauri Vijimambo iongee na Mhe. Balozi na bila ajizi Vijimambo ilipiga simu kumtafuta Mhe. James Alex Msekela lakini tukaambia ametoka tujaribu kesho yake yaani siku ya Ijumaa Oct 3, 2014 saa 3 asubuhi saa za Italy.
Vijimambo ilipotimu saa 3 asubuhi saa za Italy ilipiga simu kwa ofisi ya Ubalozi wa Tanzania nchini Italy kujaribu tena kuongea na Mhe. Balozi lakini hatukuweza kumpata na tukaambiwa yupo mkutanoni na dada muhudumu wa simu akataka kutupatia namba ya Mhe. ya kiganjani lakini baada kutuambia tusubili kidogo kwenye simu na aliporudi badala ya kutupatia namba ya Mhe. Balozi aliomba tuache namba yetu ya simu kusudi Mhe. apewe na ikibidi aweze kutupigia lakini mpaka sasa hizi hatujapata simu yeyote toka Ubalozi huo.
Vijimambo pia ilijaribu kuongea na Afisa wa Uhamiaji Tanzania ambaye hakutaka kutajwa jina lake yeye alisema inawezekana uzembe upo pande zote mbili na swala la kuchelewa kupata pasi kwa miaka miwili huu ni muda mrefu sana, Ubalozi hauandiki pasi za kusalifiria hii ni shughuli ya Uhamiaji Tanzania.
Timu ya Vijimambo inawaomba wahusika walifuatilie swala hili kwa ukaribu zaidi.
Kwa kusoma barua ya mdau nini alichokiandika kuhusu Ubalozi wa Tanzania uliopo Rome Italy Bofya soma zaidi.
UBAYA WA UBALOZI WETU WA ITALY
Tunaomba uitangaze habari hii bila kuificha na wala usipunguze hata herufi moja!!!
Kila aliyewahi
kuomba huduma toka ubalozi wetu wa Rome
ana malalamiko yake.Ima atakuwa amecheleweshwa mno kupatiwa huduma hiyo au hakupatiwa
kabisa.Muda mrefu tumenyamaza kimya tukitegemea kuwa hali ingebadilika, lakini
kila siku zinavyokwenda mambo ndivyo yanavyozidi kuwa magumu na
kuharibika hasa katika kipindi cha miaka miwili iliyopita.
Kutozingatiwa
matatizo yetu limekuwa ni jambo la kawaida mno kiasi cha kutufanya tujiulize
mara mbili.. Sisi kweli ni raia wa Tanzania wenye haki ya kupatiwa msaada toka
ubalozini kwetu?
Mara zote msaada
tunaokuwa tukiuhitaji SI PESA, kiasi cha kwamba Mh.Balozi aseme kuwa nchi yetu
haina uwezo wa kipesa kusaidia raia wake.Msaada tunaoomba ni KUPATIWA VYETI
HUSIKA ILI NASI TUWEZE KUKAMILISHA HATI ZA UHALALI WA UKAAZI WETU.
Matatizo yetu yana
sehemu tatu kuu zifuatazo:
1. Hivi sasa watu wengi pasi zetu zinaisha
2015 na tumeshamuomba Mh.Balozi amtume Afisa
wa pasi-japo kwa gharama zetu - aje kututatulia tatizo hilo HAJAFANYA LOLOTE.
Mh.huyo katuimbisha kuwa angemtuma Afisa wa pasi August au September, kuja kuonana nasi na
miezi hiyo imeshapita na hatuoni dalili zozote za kusaidiwa. Kuna hatari kubwa
ya wengi kutokuwa na valid passports ifikapo 2015, Je tutawalaumu watu
watapotumia njia za kienyeji na za vichochoroni
kutatua tatizo lao?
2. Kuna watu wameomba pasi imeshapita sasa
miaka miwili na
stakabadhi za malipo wanazo na wala hakuna jibu lolote la maana wanalopewa.
3. Tuna watoto wetu waliozaliwa huku hawana
pasi wanashindwa kusafiri na wazazi wao kuja
Tanzania. Ubalozi unashindwa vipi kutoa huduma japo mara moja kwa mwaka?
Tunaamini
udhalilishaji huu unatokana na filosofia ya Mh Balozi ya kutojali watu anaowaongoza
maana inajulikana hata huko mikoani alipokuwa (Dodoma & Mwanza) wananchi
hakuwa akiwajali.Tunahofia asije akawa anataka kuendeleza mfumo huo hata huku ughaibuni.Mbona
Mheshimiwa Rais Kikwete yupo very simple? Anajali na huwatembelea raia wake mara
kwa mara?,Hata misiba ya raia wa kawaida huwa
anahudhuria, sasa huyu Balozi yeye ni nani? Je yeye anajiona ni bora
kuliko Rais wetu?.
Tumelazimika kueleza
yote haya si kwa sababu tunataka tu kulalamika LA HASHA, bali tumeona
tukiendelea kuficha, kilio kitatuhusu. Yes ..KI - TA - TU - HU - SU.
Tunaviomba vyombo vyote vya habari vifikishe udhalilishaji huu
kwenye idara husika hasa Bungeni na kwa Mheshimiwa Rais ili
waelewe kuwa UBALOZI WETU WA ITALY HAUJALI WATANZANIA.UNAJALI MASLAHI YAO
YA KIBINAFSI.
LABDA TAARIFA HII
ITAZIAMSHA BALOZI NYINGINE ZIWEZE KUWAJALI RAIA WA TANZANIA.SISI TUNAJIVUNIA
URAIA WETU HATA KAMA BALOZI HATUJALI NA TUNAIPENDA NCHI YETU NA TUTAENDELEA
KUIPENDA NA KUITUKUZA.TUTAFURAHI KUONA
NA MABALOZI WETU WANAELEWA UMUHIMU WA KUWAJALI WATANZANIA KULIKO MASLAHI YAO YA
KIBINAFSI.
Imeandikwa na :
(WAKEREKETWA WA UTURUKI,UGIRIKI, NA ITALY
4 comments:
They should contact homeland security on the ground
Homeland security ya wapi? TZ, Italy au Uturuki?
Naona wewe unaubaya na huyu Balozi, amekukosa nini? Mbona wengine tunapata huduma! Tena jamaa mambo yake fast kweli na yuko simple sana, na ametembelea hadi sehemu ambazo wala hatumtarajia. alifika hata huku Ugiriki na akaomba yeye mwenyewe kukutana nasi. Kwa kujibagua kwa baadhi ya Watanzania, wengine hakuja na baadaye wanataka ratiba zao binafsi. Jamani, tuwaheshimu viongozi wetu na tuwape ushirikiano. Nijuavyo mimi safari ya Afisa wa pasipoti kuja Ugiriki inaandaliwa na wanatarajia kuja na maafisa kutoka Dar. Tuache ubaya, kama baadhi mnataka siasa basi tangazeni majina yenu mkiandika, kama ni kweli basi unaogopa nini kutaja jina lako?
wewe anonymos wa hapo juu kwa nini usitaje jina lako ?Umejuaje kama inaandaliwa safari ya kwenda ugiriki na maafisa kutoka Dar?Au unatumiwa kutawanya propaganda ili yaonekane madai ya wakereketwa si ya kweli? Suala kuu hapa si kuleta siasa wala kuvunja heshima kwa viongozi, bali ni kilio cha kutafuta msaada baada ya kuona ahadi nyingi zisizotekelezwa.
Post a Comment