Aliyekuwa mjumbe wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Prof. Mwesiga Baregu, alisema lengo la kuundwa kwa Ukawa lilikuwa ni kuunganisha nguvu kusaidia mchakato wa kupatikana kwa katiba mpya ambayo alidai kupinduliwa.
Prof. Baregu, alisema maazimio ya Ukawa yatasaidia kuunganisa makundi mengine yaliyokuwa ndani ya Bunge Maalumu la Katiba ambayo yalikuwa na nia moja na umoja huo, hivyo kutia nguvu baadaye.
“Lengo ni zuri, wanahitaji kujipanga upya. Ni uamuzi ambao utaimarisha vyama vya siasa hapo baadaye. Itasaidia katika vuguvugu hilo la katiba mpya kwa kuunganisha asasi za kiraia na wale ambao hawakuridhika na mchakato wa katiba mpya. Itasaidia kuwaunganisha Ukawa na Watanzania kwa ujumla,” alisema.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Tanzania (Jukata), Deus Kibamba, alisema: “Mimi ninaafiki, wanaweza wakaleta ushindi mkubwa sana, kwani ninavyoamini umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu.
Kwa mujibu wa Kibamba, Ukawa wakifanikisha kutekeleza malengo hayo, wapigakura katika chaguzi zijazo watakuwa na hamasa kubwa na kutafanya vyama vingine vya siasa ambavyo havikuungana na Ukawa kuweza kufutika kwa kutolea mfano kwa Marekani.
Rais wa zamani wa Chama cha Wanasheria Tangayika (TLS), Francis Stolla, aliunga mkono hoja hiyo, kwa kusema: “Sasa hakutakuwa na kugawana kura. Wakitekeleza kweli, litaweza kuleta mafanikio makubwa kwa chaguzi zijazo.”
CHANZO: NIPASHE
1 comment:
Asanteni sana Ukawa, tatizo kuuuuubwa tulilonalo NI mbinu kubwa za CCM ZA kuiba kura wamekubuu kwa huo wizi je mmejipanga vipi kuukabili kwa maana wameshaanza, kama waliweza kubadili muundo wa maoni ya katiba na kuupitisha wanavyotaka je uchaguzi utakuwaje, hii ni aibu tupu. Fedha zimeanza kutembezwa kila kona na wanaotaka kuwania je hii ni halalali. Pili na Ukawa kuweni makini katika uteuzi wenu wa mgombea, muhimu awe mwenye umri unaokubalika na sio miaka 70!! Tuko pamoja.
Post a Comment