Advertisements

Sunday, October 19, 2014

VIJANA WA VYUO VIKUU WAMKUMBUKA MWALIMU NYERERE

 Katibu Mwenezi wa CCM Tawi la Chuo Kikuu Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Rehema Akikweti akisoma salaam za ufunguzi wa mkutano wa Vijana wa Vyuo Vikuu wa CCM kuadhimisha Kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa.
 Sehemu ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu wakisikiliza mada mbali mbali

 Mwenyekiti wa UVCCM tawi la chuo Kikuu cha Dar es Salaam Theodora Malata akisoma risala ya Umoja wa Vijana wa Elimu ya Juu.

 Katibu Mtendaji wa Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu Tanzania Ndugu Christopher Ngubiagai akihutubia wakati wa kongamano hilo.
 CCM Oyee!
 Sehemu ya wanafunzi wa Elimu ya Juu wakisikiliza kwa makini mada mbali.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia Vijana wa CCM kutoka vyuo Vikuu mbalimbali kwenye Mkutano wa Kuadhimisha Kumbukumbu ya Baba wa Taifa uliofanyika Mlimani City.
 Wanafunzi wakiwa kwenye ukumbi wa mikutano Mlimani City kwenye  mkutano wa Vijana wa Vyuo Vikuu wa CCM kuadhimisha Kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa.
 Zeyana Mohamed Haji Katibu Uchumi na Fedha Mkoa wa Vyuo Vikuu Zanzibar akizungumzia kuboreshwa kwa Elimu ambayo itakomboa Watanzania.
 Gulatone Masiga akizungumzia ubora wa Rasimu iliyopendekezwa na BMK dhidi Rasimu ya 2 ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
 Steve Nyerere akizungumza wakati wa mkutano huo ambapo alisema wakati umefika kwa wasanii wa kitanzania kula milo mitatu kutokana na kukumbukwa kwenye Katiba iliyopendekezwa.
 Raymond Mweli kutoka chuo Mzumbe akizungumzia  falsafa za Mwalimu Nyerere juu ya Katiba ya CCM.
 Wanafunzi wakirekodi matukio kwa kutumia simu zao.
 Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Ndugu Philip Mangula akihutubia Vijana wa Vyuo vya Elimu ya juu kwenye kongamano la Vijana  lililofanyika Mlimani City jijini Dar Es Salaam.
 Nasra Khalfani akipokea kadi yake ya uanachama wa CCM
 Vijana wakila kiapo cha uanachama wa CCM
 Justin Mushi akikabidhi kadi yake ya Chadema kwa makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula na kutangaza kujiunga rasmi CCM.
(Picha na Adam Mzee )

No comments: