Uongozi wa Jumuiya ya Watanzania DMV ukifanya kikao na kamati zake mbalimbali ndani ya uongozi wa jumuiya hiyo kujadili maswala ya wanajumuiya wake yakiwemo maswala ya afya, ukusanyaji wa ada za uwanachama ikiwemo kutengeneza vitambulisho maalum vya mwanachama na njia mbadala za kuongeza kipato kwenye Jumuiya ya DMV. Swala lingine lililojadiliwa ni kuangalia na kuwatambua Watanzania wenye nafasi kwenye jamii kama vile Madaktari, Manesi, wanasheria na wengineo ambao wapo tayari kushirikiana na jumuiya, kwa kufanya hivyo jumuiya itathamini mchango wao bila kujali uanachama wake.
Uongozi wa jumuiya ya Watanzania DMV ukikutana na kamati mbalimbali ndani ya uongozi wa jumuiya hiyo kilichofanyika Jumapili Oct 19, 2014. Waliohudhuria kikao hicho ni Rais Iddi Sandaly, Makamu wa Rais Hariett Shangarai, Katibu Said Mwamende, Dr Hamza Mwamoyo, Makamu Katibu Bernadeta Kaiza, Harun Ulotu, Dr. Mohamed Olotu, Charles Lawa, Mary Kombe, Mathias Choma, Benjamin Mwaipaja, Asha Hariz, Asha Nyang'anyi, Joha Nyang'anyi, Raymond Abraham, Genes Malasy, Julia Shirima, Jennifer Julius, Gerald Mude na Joyce Cottrell.
Kikao kikiendelea
Wanakamati wakifuatilia kikao.
Joyce Cottrell kamati ya Afya akifuatilia kikao
kwa picha zaidi bofya soma zaidi
1 comment:
Vipi? Hawana sehemu ya kufanyia mkutano?
Post a Comment