Advertisements

Monday, October 6, 2014

WANAFUNZI ALBINO WALIOPO BWENINI WAHOFIA USALAMA WAO

Wanafunzi wa bweni ambao ni walemavu wa ngozi na wasioona wanaohifadhiwa na serikali katika shule ya msingi pongwe jijini tanga wameiomba Serikali kwa kushirikiana na wasamaria wema kuwajengea uzio shuleni hapo kufuatia kutembea umbali wa mita 100 wakati wanapokwenda kujisaida nyakati za usiku hatua ambayo inahatarisha usalama wao.
Wakizungumza shuleni hapo wakati wasamaria wema walipokwenda kuwasaidia wanafunzi walemavu wa ngozi na vipofu vifaa mbali mbali ikiwemo vya kusaidia walemavu wenye uono hafifu,wanafunzi hao wamesema wameanza kuingiwa na hofu ya kuuawa kufuatia nyakati za usiku na kulazimika kwenda nje ya mabweni yao kujisaidia ambayo yapo umbali wa mita 100 kutoka eneo wanalolala ambako hakuna uzio.
Kwa upande wake mwalimu wa mlemavu asiyeona anayefundisha shule hiyo maalum Bwana Jumaa Mwachalika ameiomba serikali kuharakisha zoezi la kuwaingiza katika teknlojia ya tehama kwenye masomo yao kwa sababu wangepata vitendea kazi ikiwemo kompyuta maalum kwa watu wasioona vingeweza kuwasaidia kufanya vyema kuanzia elimu ya msingi hadi vyuo.
Kufuatia hatua hiyo baadhi ya wasamaria wema waliojitokeza kuwasaidia walemavu hao vifaa mbali mbali ikiwemo mashine za kuwaongezea uwezo walemavu wenye uono hafifu,wameiomba jamii kujitokeza kusaidia walemavu hao kutoka mikoa mbali mbali nchini ambao wamehifadhiwa katika shule hiyo ya bweni kutokana na sababu za kiusalama kufuatia wenzao walemavu wa ngozi kuuawa kikatili na baadhi ya watu.

No comments: