Advertisements

Thursday, November 27, 2014

Bi harusi wa miaka 14 ampa sumu mumewe

Bi harusi wa miaka 14 nchini Nigeria (sio huyo kwenye picha) ameshtakiwa kwa kuwaua watu wanne akiwemo mumewe wa miaka 35 baada ya kuweka sumu ya panya katika chakula alichoandaa kwa sherehe za haruysi yake.

Kesi hiyo imewashangaza wahaharakati wa haki za kibinaadamu ambao wamesema kuwa msichana aliyeozwa kwa mume aliye mara mbili umri wake anafaa kuchukuliwa kama mwathiriwa na wala sio muhalifu.

Wasila tasiu kutoka familia masikini katika eneo la waislamu la kazkazini huenda akakabiliwa na kifo iwapo atahukumiwa.

Shahidi wa kwanza wa kiongozi wa mashtaka Lamido Abba Sorron-Dinka alikuwa msichana wa miaka 7 anayejulikana kama hamziyya,ambaye alikuwa akiishi katika nyumba moja na Tasi'u pamoja na mumewe Umar sani,wakati bi haru huyo alipoweka sumu ya panya katika chakula hicho.

Hamziyya alijulikana tu kama dadaake mke wa kwanza wa bwana Sani,mwanamke aliyeolewa na marehemu awali katika eneo ambapo ndoa za wake wengi zimekithiri.

Msichana huyo wa miaka 7 alisema kwamba Tasi'u alimpa fedha ili kununua sumu ya panya kutoka duka moja jirani mnamo tarehe 5 mwezi Aprili,siku ambayo bwana Sani alifariki.

''Alisema kuwa panya wanamsumbua katika chumba chake'',Hamziyya aliiambia mahakama.Upande wa mashtaka baadaye ulisema kuwa badala yake Tas'u aliweka sumu hiyo ya panya katika chakula ambacho alikuwa amekiandaa kwa sherehe za baada ya harusi kwa kuwa alijuta uamuzi wake wa kumuoa bwana Sani.

Msichana huyo alikataa kuzungumza mahakamani.

Jaji Mohammed Yahaya,katika mahakama ya Gezawa alitoa hukumu kwamba Tasi'u ambaye alikataa kuongea katika mahakama hana hatia katika kusikizwa kwa kesi mnamo mwezi Octoba ambapo alisomewa mashtaka.

Jaji huyo alikataa ombi la upande wa mshtakiwa la kesi hiyo kupelekwa katika mahakama ya watoto.

Ushahidi wa Hamziyya uliungwa mkono na Abuwa Yussuf muuzaji duka katika mji wa Unguwar Yansoro ambaye alithibitisha kuuza sumu hiyo kwa mtoto huyo.

Jirani ya Bwana Sani mwenye umri wa miaka 30 ambaye ni mkulima, Abdulrahim Ibrahim alitoa ushahidi ambapo alisema kwamba alipewa chakula hicho kilichopikwa na Tasiu.''Nilipoletewa chakula hicho niliona vipande vipande vyeusi''aliiambia mahakama.

Alikula vipande vinne vya madonge vilivyotengezwa na maharagwe lakini hakupendelea ladha yake'',alisema na kuongezea kuwa ni Umar pekee aliyeendelea kula.

Baadaye alisema kuwa alimuona bwana Sani katika bustani ,akiwa mgonjwa na kumpeleka nyumbani.

Lakini alipokuwa akijaribu kumuuguza bwana sani ,aligundua kwamba watu wengine watatu ambao walikuwa wamekula chakula hicho wamefariki kwa ghafla.

Viongozi wa mashtaka walidai kwamba chakula cha Tasiu kilichowekwa sumu kiliwaua watu wanne na hivyobasi kuwajumuisha wanne hao katika kesi moja ya mauaji.

Nigeria haijawahi kumyonga mtoto aliyefanya uhalifu tangu mwaka 1997,ambapo taifa hilo liliongozwa na dikteta Sani Abacha,kulingana na shirika la kibinaadamu la Human Rights Watch.

BBC

4 comments:

Anonymous said...

kama si huyu kwenye picha kwanini umeiweka hii picha halfu watanzania mnependa sana kuwasema waafrica wenzengu wasio watanzania.you better stop that shit.i lived in Tanzania for so long and I know Kiswahili very well and you guys you got a lot of issues in your country that are so bad why don't you talk about it.
afadhali sisi we got our African cultures and we live by them.

Anonymous said...

That's culture to marry 14 years old? Live you're crap

Anonymous said...

you must be a very ignorant Tanzania dude,your white bosses that you worship they used to walk in London street as well in u.s.a to get prostitute who were 9 years only now they act like a civilized nations. you don't read history you don't know anything that surround the world that you live and worship you white bosses no wonder you came up with ignorant comment.
at least we NIGERIANS MARRY THEM.Hatuwatumii wanawake wetu ovyoo kama nyinyi watu wajinga sana msiokuwa na African cultures.you copy anything that white man pass over to you.Get you own africa identity and stop copy white man cultures.wajinga wakubwa sana sana sana.

Anonymous said...

Iam coming to Tanzania again and i want to marry you sister this time,i dont want her to stay and live that kind of life of depression without a really african man in her life. trust me i know you very well.nitakuja kumuowa dada yako wa mwisho i dont care how young she is i will trust me and you will start respecting me as you shemeji mwenye mali nyingi sana.