Advertisements

Saturday, November 1, 2014

HAKA KAUJUMBE KAMENIGUSA WE MWENZANGU VIPI UMESALIMIKA HUKO

LIFE BEGINS AT 40! So how old are you?

Huo ni msemo wanao waingereza.
Today is your future kwa taarifa yako.. Ulipokuwa mdogo ulisema nikiwa mkubwa nitakuwa na gari na nyumba nzuri wazazi wangu wataishi hivi na vile. Je unayo? Je imetokea? Maybe yes. But maybe no.
Kama haijatokea je bado hujawa mkubwa? Basi kama ni mkubwa ujue kuna kitu hujafanya.

Utasema tena nikifika miaka 40 nataka niwe na hiki na kile watoto wangu wasome international skul nk. Subiri uone miaka inavyoenda. Usishangae kufika 40 bado umeajiriwa kwa mtu na anakugombeza kwa nini mwanao anaumwa kila siku unachelewa kazini. Kazi nyingi. No bright future. No enjoyable present. Just existing and not living!
Hapo ndo unawaza kufuga ng'ombe wa maziwa kibamba kwenye kiwanja chako cha miguu 12 kwa 15! Wenzako wa umri wako hapo unasikia wameanzisha bness in Australia. Wamenunua kiwanja Mbezi Beach kwa 300M! Wanamiliki Apartment Johannesburg. Wakienda UK wanaenda kula The Ritz (Google that). Wanasomesha watoto zao the finest schools available wewe wa kwako wakati huo wamekosa nafasi Makongo wameenda Kibamba Secondary School wanapanda daladala sita kwenda na kurudi full kutukanwa na makonda.

Wenzako in their 40s wanasaidia wasio na uwezo katika jamii wewe ndo kwanza ukipokea simu kutoka kijijini una-mute! Wenzako in their 40s wakisikia kuna ujenzi wa nyumba ya ibada wanachangia 5M kimyakimya.. Wewe ukitoa laki moja basi mpaka mtaa wa saba watakujua! Halafu unashangaa wanazidi kuinuliwa. Mwenye nacho ataongezewa au hujui? Na asiye nacho..... (Malizia)
Wenzako in their 40s wana exposure ya uhakika. Walishafika kuanzia Sauzi, Botswana, Mozambique, Kenya, Ethiopia, Ghana, Naija, mpaka Egypt, The UK, Australia, Hawaii, Mexico, Croatia, The Netherlands, Switzerland, US, Panama mpaka Puerto Rico, Brazil na jirani zake, Hong Kong, Australia, Japan, China, (Incredible) India, Thailand, Singapore, New Zealand, Comorros, you name it..!! Wewe hata Kampala hujawahi fika. Kila siku Tegeta Posta ndo ruti yako miaka 15 mfululizo eti unatafutia watoto maisha! Unaishi au unaisha?

Acha mawazo mgando. Hiyo ajira ifanye serious sana tu lakini kwa muda tu. Jiandae kusimama mwenyewe. Kwani hujiamini? Na Mungu naye humwamini? Changamoto ni sehemu tu ya kufika kileleni. Don't be afraid. Don't dwell in that comfort zone!! Unasubiri kiinua mgongo? Utaenda kukiinvest wapi na kwa nguvu ipi. Na utaenjoy retirement kweli kama at 60 yrs ndo unafungua duka la vifaa vya ujenzi eti vinalipa. Kwa nini hukufungua ukiwa 30 ili uone vinalipa au la. At 60? With due respect.

Suffer the pain of discipline now. Or else you will suffer the pain of REGRET. Halafu ukianza kuregret ndo pressure zinakuja, stress, nk mwisho unawacha hata hao watoto in a far worse situation than your own lifetime.

Life Begins at 40 my friend.. How Old Are You?

Inbox me tushauriane fursa inayoweza kukupa hayo unayoona leo kama ndoto.
Kamata fursa #twenzetu!

Have a Simple Saturday.

7 comments:

Anonymous said...

Acha kujilinganisha na wengine wewe! nani kakwambia itakusaidia? Fanya kazi kwa bidii zaidi au iba kwa bidii zaidi, whichever one suits you. To each their own, ok?

Anonymous said...

Wewe mwenye kuandika hii hivi watu wote wangekuwa sawa nani angemfanyia kazi mwingine??? Cha pili hao unaowasema wana maisha je unajua pesa walizipataje! ? Au unataka watu wajenge maghorofa kwa kuuza madawa na kuua watoto wa watu ilimradi mtu aendelee??? Au kuiba labda kazini au kwa njia yoyote ili ujue mtu ameendelea?? Soma history ya matajiri duniani uone walikoanzia!! Kwa taarifa wenye pesa safi wamzipata karibu na kustaafu!! Pesa chafu ni ile haina baraka na hailast!!!

Anonymous said...

Huwezi kujilinganisha na mtu mwingine kwani hujui amevipata wapi wengi ni wezi tuu .Na wale ambao hawajui watalisha nini watoto wao
utamfananisha na muuza unga au mwizi wa serikali?Just count your blessing

Anonymous said...

Naona anonymous wengi hapo juu imewatachi sababu mnasagarhumba na wengi mpo ughaibuni,40 ndo hiyo wake up!

Anonymous said...

Watu wote si sawa na hakuna fursa sawa kwa wote. Wewe unapanga kutembela Hawaii, mimi najitahidi niende Zanzibar na familia angalau mara moja katika miaka mitano.
Hatulingani ila ni muhimu kila mmoja akajitahidi kwa mazingira yake. Nakubaliana nawe kwa point moja tu, kama kuna unaloweza kufanya sasa, usi subiri, jaribu kualifanya sasa (as long as you have a plan B)
Siku hizi kila mtu ni expert wa maisha na mafanikio. Mlikuwaga wapi enzi hizo?

Anonymous said...

Hahahahaha, jamani mbona hasira kali kali khaaaa!!! Kwa mtizamo wanfu naona kama hii ni mada tu ambayo muandishi ameiandika iwe kama changamoto au motivation kwa watu. Hajasema kama wewe inakuhusu au yeye anajilinganisha. Tatizo moja wapo ambalo wa Tanzania tunalo basi ni hili na daima gatutiendelea wala kusonga mbele kama tunaishi namna hii. Yaani mie nimeisoma tu hii mada nikasema yes, this is a nice motivation to us. Baada ya hapo nikajiuliza how old I am and what have I done so far. Baadae nikapeleka umri mbele ki fikra na nikasema na nikifikia hio 60's nitakuwa wapi kimaendeleo. Acheni majungu na kijinga jinga na mu focus on postive aspects instead of negative. Pongezi kwako muandishi wa hii mada. Umenifungua sana upeo wangu wa akili kwa kutaka kufanya kazi kwa bidii anf achieve the best at the desired age.

From Canada

Anonymous said...

Mkuu Mada nzuri lakini umepotosha kidogo au umeikuza sana.nijuavyo mimi au nilivyosikia at 40's atleast uwe umefanikiwa haya ( kwa wanaume tu)
1: atleast 2 kids kama ni rijali
2: umeshaoa
3:uwe una biashara binafsi kama Si muajiliwa
4: uwe na cheo atleast supervisor kama umeajiliwa.
5:unaishi kwako au una kibanda Chako cha atleast vyumba 3
Yani kama uko 40's then, Huna hivyo vitu ujue jua limezama ndugu yangu

hivyo ni vitu minimum kabisa, ndio maana nimetangulia kusema mtoa mada amepatia lakini kawatisha wadau.

it's just my opinion
Thanks