“Nimepokea kwa mshtuko na masikitiko taarifa za vifo vya watu 12 waliopoteza maisha papo hapo na kusababisha simanzi kubwa kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki zao, huku taifa likipoteza nguvu kazi muhimu kwa maendeleo yake kutokana na ajali za barabarani,” alisema.
Aliwaomba wote waliopoteza ndugu zao katika ajali hiyo wawe na moyo wa uvumilivu na subira katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo. Wakati huo huo, polisi mjini hapa inamtafuta dereva wa basi la Kampuni ya Super Aljabir lilogonga treni ya Tazara kwa uzembe na kusababisha vifo vya watu 12 na majeruhi 44.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Leonald Paul, alisema polisi kwa kushirikiana na wananchi inamtafuta dereva wa basi hilo aliyetoweka eneo la tukio la ajali baada ya kusababisha uzembe wa kutochukua taadhari katika eneo ya makutano ya reli licha ya abiria kumtahadharisha.
Kamanda Paul alimtaja dereva huyo kuwa ni Kasim Ndela (35) aliyekuwa akiendesha basi hilo lenye namba za usajili T725 ATD Scania mkazi wa Morogoro ambaye anadaiwa kuwa chanzo kikubwa cha ajali hiyo baada kuvuka kwa makusudi reli kuwahi kupita eneo.
Alisema kuwa basi hilo ambalo likuwa likitoea Morogoro kwenda Ifakara lilipofika katika eneo hilo liligongwa kwa nyuma na treni na hatimaye kupoteza uelekeo na kuanguka kisha kusababisha vifo vya watu hao pamoja na majeruhi.
Kamanda Paul amewataja waliokufa na kutambuliwa kuwa ni pamoja na Fulgence Usangila (60), Alberta Usangila, (62) Binti Usangila (68), wote wakazi wa kijiji cha Ichonde- Mangula, Joseph Kazwila Maganga (34), mkazi wa Sinza Dar es Salaam, Latifa Joshua (5), Asha Mnyatwiru (38), Said Bwakumbwaku (40) na Nuru Joshua (6), wote wakazi wa Ifakara.
Kamanda Paul alisema kuwa miili minne haijatambuliwa na imeifadhiwa katika hospitali teule ya Mt. Francis, Ifakara.
Majeruhi wanaoendelea na matibabu ni pamoja na Kalonga Mahenda (6), mkazi wa Kijiji cha Mngeta, Zebi Makalius (44), Chita, Maria Kipeta (45), Ichonde Joyce (20), mkazi wa Njombe, Maria Ngoloma (35), mkazi wa Mahenge, Nyamtondo Juma (28), mkazi wa Kamnyonge, Willy Ndelemia (20), mkazi wa Nzega, Beatha Usangila (75), mkazi wa Ichonde,Catherine Peter (53), mkazi wa Dar es Salaam, Teresia Elias (60), Kihonda Morogoro, Naomi Malela (22), mkazi wa Sululu, Felisa Sauli (28), mkazi wa Itete, Ulanga.
Wengine ni Gaudensia Sotela (22), Sai Zengo (42), wote wakazi wa Chita, Cosmas Nduye (53), Ludiiki Livangala (62), Mtimbila Shukuru Mwaikambo (25), Muuguzi mkazi wa Mlabani, Minza Charles (26), Shinyanga, Sikujua Rashid (19), Geita Kilangali (37), mhasibu mkazi wa Geita.
CHANZO: NIPASHE
3 comments:
Asante Mheshimiwa Raisi wetu,! La msingi kabis ni serikali ya Tanzania kujali na kutengeneza barabara zetu ziwe na hadhi ya kueleweka! Sio kwamba fedha hatuna, ! rasilimali tulizo nazo ni nyingi saaana. Achana na hizo hivi ni kiasi gani cha fedha kilichotumika kwenye BUNGE LA KATIBA na bado katiba yenyewe imechakachuliwa, hivi kweli hizi salaam za pole ni za haki?? tengenezeni barabara za kueleweka na madereva wafuate taratibu na sharia. ulevi nao unachangia ajali !!!!!
Hii inakuwaje wadau, Profesa Dakta JK hayupo nchini hivi hakuna Acting President, katiba inasemaje?
Definitely someone is running the country
Post a Comment