Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Forum
CC imeandaa kongamano la siku moja kwa vijana kutoka Asasi za kiraia lililojadili msimamo wa
Tanzania juu ya masuala ya Mazingira, hususan Mabadiliko ya Tabianchi kuelekea Mkutano Mkubwa wa Mazingira Duniani
utakaofanyika katika jiji la Lima nchini Peru, Desemba 2014.
Sehemu ya Washiriki walioshiriki katika kongamono hilo la
siku moja lililoandaliwa na Taasisi isiyo ya kiserikali ya Forum CC
wakifuatilia mjadala kwa makini.
Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mh. Ummy Mwalimu (wa
pili kulia) akijibu maswali ya washiriki katika kongamano la vijana jijini Dar
es Salaam katika Hotel ya JB Belmont. Kongamano hilo la siku moja lililenga kukusanya
maoni ya vijana na kuainisha changamoto katika suala zima la Hifadhi ya
Mazingira na Mabadiliko ya Tabianchi.
Naibu Waziri, Ofisi
ya Makamu wa Rais, Mh. Ummy Mwalimu (wa kwanza kulia) akiwa katika picha ya
pamoja na baadhi ya washiriki wa kongamano hilo. Wengine katika picha,
(waliokaa) ni Bi. Grace Munna, Mkurugenzi wa Program kutoka Forum CC.
Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mh. Ummy Mwalimu
akiongea na waandishi wa habari (hawapo
pichani) mara baada ya kufungua kongamano hilo.
No comments:
Post a Comment