Mwili wa marehemu aliyefahamika kwa jina moja la Betty baada ya kupigwa risasi leo asubuhi huko Yombo Vituka, Temeke jijini Dar es Salaam ukiwa umesitiriwa kwa kufunikwa na khanga.
Gari alilokuwa amepanda marehemu betty likiwa limedumbukia mtaroni kutokana na dereva wa gari hilo mali ya kampuni ya ulinzi ya Tunu kupigwa risasi ya mkono mara baada ya kukataa kusimama wakati alipoambiwa kufanya hivyo na majambazi.
Majambazi wawili waliokuwa na pikipiki wamuua Binti mmoja aliyefahamika kwa jina la betty huko Yombo Vituka wakati binti huyo akiwa kwenye gari la kampuni ya ulinzi ya TUNU wakati wakielekea benki.. Binti huyo aliambatana na mlinzi wao aliyekuwa na silaha.
Wakati wakiwa njiani kuelekea benki ikatokea pikipiki na kuwapita kidogo na jambazi mmoja akatoa bastola na kumuamuru dereva asimame akagoma ndipo wakampiga risasi mkononi na gari kuelekea mtaloni. Dereva akanyoosha mikono kusalimu amri.
Walipomwambia yule Binti a toe pesa akawa mkaidi ndipo wakampiga risasi kichwani na kufa palepale! Inasemekana wamepora kiasi kikubwa cha pesa.
Na wakati wanaondoka kiasi kingine cha pesa walizitupa barabarani na kusababisha tafrani kwa wananchi. Tajiri alipofika na kukuta Binti yake kauwawa, alianza kulia na watu wakaanza kumtuliza lkn nae wakampora simu yake ya mkononi.
Source: Mdau Magode
No comments:
Post a Comment