ANGALIA LIVE NEWS

Monday, November 10, 2014

MASHINDANO YA MASHUA YA MERCEDES BENZ CUP 2014 YAFANA JIJINI DAR

Moja ya mashua ikisukumwa kurejeshwa katika eneo lake la hifadhi baada ya kumaliza mashindano hayo.
Mratibu wa waendesha mashua Michael Sulzar akitangaza matokeo ya mashindano ya kuwania kombe la Mercedes Benz 2014 yaliyofanyika katikati ya wiki. Jumla ya timu kumi na nne (Mashua) zilishiriki katika michuano hiyo ya siku mbili.
Waendesha mashua Al Bush na mwenzake Pugwash wakiwa na kombe la ushindi la Mashindano ya mashua ya siku mbili ya kombe la Mercedes Benz yaliyofanyika jijini Dar es salaam Yatch Club.
Mtoto wa mshindi wa kwanza katika mashua za kawaida David Scott (ambaye aliendesha mashua hiyo akiwa na Christina) akimsalimia Ofisa Mtendaji mkuu wa CFAO Motors, Wayne McIntosh kabla ya kukabidhiwa tuzo ya wazazi wake ya ushindi.
Mark Henderson na Shane Rumbold wakikabidhiwa tuzo ya uanamichezo bora, walikuwa katika Mashua Shark aina ya Hobie Tiger.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa CFAO Motors, Wayne McIntosh akizungumza kabla ya kukabidhi kombe la Mercedes Benz kwa washindi wa jumla Al Bush na mwenzake Pugwash. Michuano hiyo ilianzia na kumalizikia Dar Yatch Club Msasani. Kulia aliyebeba kombe hilo ni Meneja Masoko wa CFAO Motors, Tharaia Ahmed.

No comments: