ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, November 9, 2014

MCHEZAJI BORA WA MWEZI "SURE BOY" AKABIIDHIWA ZAWADI YAKE‏

Kaimu Katibu Mtendaji wa Bodi ya Ligi Syephen Mguto (kulia) akimkabidhi tuzo Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya Vodacom kwa mwezi Oktoba,Abubakar Salum "Sure Boy" katika sherehe iliyofanyika kwenye uwanja wa Azam, Chamazi jijini Dar esSalaam jana.Afisa Udhamini na Matukio wa Vodacom Tanzania, Ibrahim Kaude (kulia) akimkabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni 1/=mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya Vodacom kwa mwezi Oktoba, Abubakar Salum "Sure Boy" katika sherehe iliyofanyika kwenye uwanja wa Azam eneo la Chamazi jijini Dar es Salaam jana.


Na Mwandishi Wetu

KIUNGO mkabaji wa Azam FC, Salum Abubakar”Sure Boy”aliyeibuka Mchezaji Bora wa Oktoba juzi alikabidhiwa zawadi ya shilingi milioni 1/= na kombe dogo makabidhiano hayo yalifanyika muda mfupi kabla ya mechi ya raundi ya saba kati ya mabingwa watetezi Azam FC na Costal Union katika mechi ya ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara iliyochezwa nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam katika uwanja wa Chamanzi, ambapo Azam FC waliichapa Coastal Union 2-1.

Akizungumza na gazeti hili jijini Dar es Salaam juzi,Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania,Kelvin Twissa,alisema kampuni yake itakuwa ikitoa zawadi kila mwezi kwa mchezaji anayefanya vizuri.

“Ligi Kuu ya Vodacom msimu huu ina ushindani mkubwa, nasi (Vodacom Tanzania) kwa kushirikiana Bodi ya Ligi(TPLB)tumejipanga vizuri tutakuwa tunatoa zawadi kwa mchezaji anayeng’ara kila mwezi na mwezi uliopita tulitoa zawadi kama hii kwa Antony Matogolo wa timu ya Mbeya City,” alisema Twissa.

Baada ya kukabidhiwa zawadi hiyo, Salum aliyeonekana mwenye furaha, alisema; “ninawashukuru wachezaji na mashabiki wa Azam FC kwa ushirikiano wanaonipa, hii ni zawadi kwa timu nzima na mashabiki wa timu yetu.”

Aidha, Shabiki wa Azam FC Hassan Kihelelo wa kawe jijini Dar es Salaam alisema anaunga mkono juhudi zinazofanywa na mdhamini mkuu wa ligi”Vodacom Tanzania”na kusema kampuni hiyo imeonesha ukomavu na ubunifu wa hali ya juu katika kuleta maboresho ya ligi msimu huu kwa kweli inastahili pongezi kwani inafanya wachezaji wetu wanaoshiriki ligi kuu kuwa na moyo wa kucheza na kuonesha vipaji vyao vizuri na kujituma zaidi wakiwa uwanjani,alisema Kihelelo.

No comments: