Advertisements

Wednesday, November 19, 2014

Mwili wa Miss Honduras 2014 wapatikana

Miss Honduras 2014, Maria Jose Alvarado. Photo Credits: Eye of Beauty
 Habari zinazoripotiwa hivi punde na shirika la habari la AP kutoka TEGUCIGALPA, Honduras zinasema kuwa mwili aliyekuwa Miss Honduras 2014 pamoja na dada yake imekutwa ikiwa imezikwa karibu na SPA ambapo walikwenda siku ya Alhamis kusherehekea siku ya kuzaliwa ya rafiki wa kiume wa dada wa Miss huyo.
Miss Honduras 2014 Maria Jose Alvarado (19) na dada yake Sofia (23) walipotea Alhamis iliyopita, na Generali wa Polisi wa Honduras Ramon Sabillon amesema kuwa Plutarco Ruiz, ambaye ni rafiki wa kiume wa Sofia alikiri na kuwapeleka askari mahala ilipozikwa miili hiyo kando ya eneo la milima la Santa Barbara, lililo kilometa zipatazo 400 magharibi ya mji wa Tegucigalpa.
Miili ilikutwa karibu na La Aguagua Spa, ambapo walikwenda kusherehekea siku ya kuzaliwa ya Ruiz.

Soma zaidi: HAPA

No comments: