Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, alipata nafasi ya kutembelea banda la Tanzania akiwa Geneva kuhudhuria kikao cha Bodi ya " Water Supply and Sanitation Collaborative Council", ofisi zake Geneva, kwa nafasi yake kama Mwenyekiti.Kulia ni Balozi wa Tanzania katika Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Geneva, Mhe. Modest Mero.
Wiki hii, Ubalozi ukiongozwa na Mama Balozi Rose Mero umeshiriki kwenye maonyesho ya UN ya kinamama, Geneva (United Nations Women's Guild 2014), yenye lengo la kukusanya pesa za kusaidia miradi ya kuendeleza watoto wenye mahitaji mbalimbali duniani kote.
Kwenye maonyesho hayo, banda la Tanzania lilijumuisha bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na kutengenezwa nchini Tanzania ikiwa ni pamoja na kahawa, majani ya chai, khanga, vitenge, vinyago, korosho n.k
Watu mbalimbali walipata nafasi ya kujipatia chakula cha Kitanzania kama vile maandazi, chapatti, samaki wa kukaanga, maharage ya kuungwa na Nazi, chai yenye viungo vya tangawizi, sambusa, pilau, n.k
No comments:
Post a Comment