ANGALIA LIVE NEWS

Monday, November 3, 2014

Uwanja wa ndege Dar washika nafasi ya nne kwa uduni

Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Moses Malaki amesema uwanja wake umechakaa kiasi cha kukosa sifa za kuwa uwanja wa kisasa barani Afrika na dunia.

Kauli ya Malaki imekuja baada ya ripoti ya matokeo ya utafiti wa mtandao wa Sleeping in Airport uliyofanywa 2014 kuonyesha kuwa JNIA inashika nafasi ya nne kwa viwanja duni Afrika.

“Huo ni ukweli usiopingika kwa sababu uwanja ulijengwa zamani na miundombinu yake haikidhi mahitaji ya sasa…. hali ni mbaya,” alisema Malaki.

“Kiwanja kinakabiliwa na tatizo la miundombinu chakavu, vyoo visivyotosheleza na wakati huohuo kuzidiwa na wingi wa abiria, jambo linalosababisha huduma zake kuwa chini ya kiwango.

“Hatuwezi kuwa bora kwa uwanja huu… hebu fikiria uwanja uliojengwa kuhudumia watu milioni 1.2 kwa mwaka, sasa unahudumia watu 2.5 milioni, hapa lazima huduma zitakuwa chini ya kiwango na msongamo utakuwa mkubwa.”

Alisema katika kukabiliana na changamoto ya msongamano, ofisi yake iko katika hatua za kuongeza vizimba vya kugongea hati za kusafiria kutoka saba vya sasa na kuwa 21.

Alisema tayari wameshazungumza na Waziri wa Mambo ya Ndani kwa ajili ya kuongeza wafanyakazi, pia kuunganisha na kuwa sehemu moja kwa mlango wa abiria wanaowasili na wa ndani, kazi itakayokamilika wiki mbili zijazo.

Utafiti

Utafiti wa Sleeping in Airport ulitokana na maoni ya wasafiri waliopitia uwanja huo ambao walielezea na kupiga kura kuhusu huduma, miundombinu na uwezo wa viwanja hivyo kutumika kama eneo la kulala wasafiri inapobidi.

Nafasi ya kwanza kwa uduni ilishikwa na uwanja wa kimataifa wa Khartoum, Sudan ukifuatiwa na N’dijili, Kinshasa DRC na Tripoli Libya nafasi ya tatu.

Katika taarifa yake, mtandao huo ulisema Afrika ina sifa ya kuwa na viwanja vingi vyenye sifa mbaya duniani, ikiwemo uchafu wa sakafu, vyoo, vitendo vya rushwa, ukosefu wa viyoyozi licha ya joto kali, migahawa ya kawaida lakini ghali na michakato ya usalama inayotia shaka.

Mwananchi

7 comments:

Anonymous said...

It's true, big shame.

Jay said...

Ule uwanja umelaaninwa na cha kushangaza rais na mawaziri wake wanatua hapo kila wanaporudi kutoka nje wanafumbia macho ubovu wake. Uwanja vyoo vichafu, AC hazifanyi kazi, na uchafu kibao umejaa mle ndani watu wanaona poa tu. Wabongo bwana, sijuwi tutabadirika lini.

Anonymous said...

Its time to invest in the airport that serves many rather than their pockets.Where does all the tax people pay at the airport in forex go???? Perhaps privatisation is in order then shit will hit the fan

Anonymous said...

La rushwa naliamini maana juzi alisafiri mtu na mizigo ikazidi akaambiwa alipie begi 200$ na alilipa bila ya kupewa risiti na begi likaunganishwa na abiri mwengine ambae hajabeba kilo nyingi, na alipodai risit akaambiwa nendeni tuu hakuna tatizo

Anonymous said...

Huu ni ukweli usiopingwa. Hii hali ya uwanja huu wa Dar E s Salaam kweli kabisa hautakiwi kuitwa International airport kamwe na ndio maana umekuwa chanzo cha kusafirishia madawa ya kulevya Tanzania tunatia aibu. Viongozi wetu mnasafiri kila mara hapo, wajenzi wamekuja mmewatimua kwa kutaka ruswha kwanza kabla ya kazi na wakaaamua kuondoka hii ni aibu tupu.
Dj iweke hiyo.

Anonymous said...

whaoooooh!!!!!

safi sana. tunazidi kuongeza maajabu ya tanzania. na si ahyo tu kuna maajabu mengi sana il tu mengine hayatangazwi. hahahahahahahaahhhahah! ccm oyeeee!

Anonymous said...

oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee