ANGALIA LIVE NEWS

Friday, December 26, 2014

‘Houseboy’ jela maisha kwa kubaka mtoto

Mahakama ya Wilaya ya Ilala imemhukumu kifungo cha maisha mfanyakazi wa ndani, Habibu Adamu (20) baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka mtoto wa miaka sita na kumsababishia maumivu.

Dar es Salaam. Mahakama ya Wilaya ya Ilala imemhukumu kifungo cha maisha mfanyakazi wa ndani, Habibu Adamu (20) baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka mtoto wa miaka sita na kumsababishia maumivu.
Hakimu mkazi wa Mahakama hiyo, Said Mkasiwa alitoa hukumu hiyo mwishoni mwa wiki na kusema kuwa mshtakiwa ambaye ni mkazi wa Majohe, atatumikia kifungo hicho baada ya Mahakama kuridhishwa na ushahidi uliotolewa na mashahidi watano dhidi yake.
“Mshtakiwa atatumikia kifungo cha maisha ili iwe fundisho kwa vijana na wanaume wenye tabia za kikatili kama hizi dhidi ya watoto,” alisema na kuongeza kuwa ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na mashahidi akiwamo daktari ndiyo uliomtia hatiani.
Kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo, Mahakama ilimpa nafasi mshtakiwa kujitetea.
Katika utetezi wake, alisema anaumwa vidonda vya tumbo, hivyo anaiomba Mahakama imhurumie kwa kupunguzie adhabu.
“Hakimu naomba Mahakama yako inipunguzie adhabu, nina vidonda vya tumbo,” alidai mshtakiwa.
Hata hivyo, Mahakama hiyo ilitupilia mbali maombi hayo na kumhukumu kifungo cha maisha jela.
Awali, Wakili wa Serikali, Silvia Mitanto aliiomba Mahakama hiyo kutoa adhabu kali dhidi ya mshtakiwa kutokana na kuongezeka kwa kwa vitendo vya ubakaji dhidi ya watoto wadogo.
Mitanto alidai kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Septemba 2013 katika eneo la Majohe Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam.
Mwananchi

No comments: