Sunday, December 7, 2014

IDRIS ASHINDA BBA


Mshiriki kutoka Tanzania aliyewakilisha ndani ya mjengo wa Big Brother ‘hotshots’ , Idris Sultan.

Aliyekuwa mshiriki wa Tanzania kwenye mjengo wa Big Brother Idris Sultan ameibuka mshindi wa shindano hilo na kuileteaheshimaTanzania, Idris pia amejishindia kitita cha dola 300,000 (Sawa na 510,186,000).

Idris aliweza kutabiriwa na wadau wengi kuwa angeweza kuibuka mshindi kutokana na wadau wengi kuvutiwa na staili ya maisha aliyokuwa akiishi katika nyumba hilo la big brother lililoko huko Afrika Kusini.

Idris amekuwa kivutio kwa raia wa nchini Nyingi sana hususani afrika nzima na kuweza kumpigia kura na hatimaye kuibuka mshindi.

Hongera Idris umeendelea kuiwakilisha vyema Tanzania mara baada ya siku kadhaa tu Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya Diamond Platmun Kuibuka na Tuzo tatu za Channel O huko Afrika Kusini

No comments: