Advertisements

Tuesday, December 23, 2014

MAKOSA MANNE YA MSINGI KATIKA HOTUBA YA RAIS.

Na   Bashir  Yakub
TAREHE 22 / 12 / 2014  majira ya  jioni rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Jakaya Mrisho Kikwete amelihutubia taifa kupitia wazee. Amezungumzia mambo mengi ila nitapitia moja tu la kashfa ya Escrow.  Habari ya Escrow ni ndefu na ina mambo mengi mchanganyiko na ya kiufundi sana.  Pamoja na kuwa mambo mengi ni ya kiufundi bado ukitulia vizuri  na kulipitia kwa umakini sakata hili  unaweza kutoka na mambo  machache lakini yenye kueleweka zaidi kiasi ambacho unaweza kumuelewesha hata mtu wa kawaida akakuelewa. Kutokana na hilo nataka  nieleze kwa ufupi wenye kueleweka dondoo chache kutoka hotuba ya rais kuhusu Tegeta ESCROW akaunti.

( 1 ) KULIKUWA    NA   PESA   UMMA.
Sijui kwanini Rais amerudia kusema kuwa pesa hazikuwa za umma. Katika mambo ambayo hayana utata katika jambo hili ni hili swali la pesa kuwa za umma au lah. Ni kitu chepesi sana kupata majibu ya swali hili lakini sijui kwanini  viongozi hasa rais na Waziri Mkuu hawataki kulielewa. Sijui ni kwa makusudi  au  kwa kulinda heshima kwakuwa serikali ilishakuwa na msimamo huo tangu mwanzo
kabla hata  ya skendo yenyewe. Nafikiri ni kulinda heshima. Rais amesema pesa ile haikuwa ya umma halafu baadae akasema kulikuwa na  kodi ya serikali ambayo haikulipwa na akasema tayari mamlaka ya mapato wameanza kufuatilia kodi zile  na  kuwa IPTL wameshakubali kulipa. Nini maana ya kauli hii na ni maana ya kauli kuwa hakukuwa na pesa ya umma.Kama hakukuwa na pesa ya umma TRA wanadai hela ya nini na kwa ajili ya nani. Kama rais angesema kulikuwa na pesa ya mwekezaji pamoja na ya umma kingeeleweka zaidi. Haiwezekani ukasema hakukuwa na pesa ya umma halafu ukasema kulikuwa na kodi ya serikali ambayo haikulipwa. Hilo ni moja.

(  2  ) MAHAKAMA   KUU   HAIKURUHUSU    PESA   ITOLEWA  KWA  IPTL
Rais amesema  mahakama iliruhusu  pesa itolewa kwa IPTL. Mahakama haikusema hivyo. Kwanza ieleweke kuwa mgogoro uliokuwa mahakama kuu ya Tanzania mbele ya jaji Utamwa si kati IPTL  na Tenesco. Mgogoro  uliokuwa  kwa Jaji Utamwa ni kati ya Mechmar na VIP Engineering. Hili hata rais mwenyewe amekiri kuwa  Rugemalira ambaye ndiye VIP Engineering  ndiye aliyepeleka mgogoro huo mahakamani kulalalmikia  mwekezaji mwenzake Mechmar.  Wakati mgogoro huo ukiwa mahakamani VIP Engeneering  ambaye ndiye alikuwa mlalamikaji aliamua aachane na mgogoro na auze  hisa zake kwa  mechmar ambaye  ndiye aliyekuwa akilalamikiwa. Mahakama kuu baada ya kuona  wenye kesi wamekubaliana  ikasema kuwa  kama wamekubaliana kesi imeisha na mambo yote kuhusu  IPTL  yakabidhiwe kwa Mechmar.Ikumbukwe IPTL inaundwa na watu wawili Mechmar na VIP Engineering ambao ndio walikuwa na kesi. Hivyo mahakama kusema hivyo ilimaanisha kuwa  mali zilizokuwa zikimilikwa na VIP Engineering zikabidhiwe  kwa  Mechmar ili abaki mmiliki wa IPTL peke yake.  Kwa hiyo Mechmar akabaki ndiye mmiliki pekee wa IPTL. Kumbuka kuwa Tanesco hakuwa anahusika kwa namna yoyote katika mgogoro huo kwa kuwa haumhusu. Maana ya hili ni kuwa mgogoro wa wa IPTL  na Tanesco haukuwa umeguswa kwa` namna yoyote na hukumu hii ya mahakama ambayo ilikubnali wenye kesi kumaliza tofauti zao. Kama haukuguswa kwa`namna yoyote ile  basi hata ESCROW Akaunti ambayo inatokana na mgogoro kati ya Tanesco na IPTL na si Mechmar na VIP Engeneering waliomaliza kesi pia haikuguswa na hukumu hiyo. ESCROW akaunti ilikuwa kwa ajili ya mgogoro wa IPTL  na Tanesco  na si mgogoro wa Mechmar na VIP Engineering. Hukumu ambayo ingetoa zile pesa ni hukumu kati ya Tanesco na IPTL na si hukumu kati ya  Mechmar na VIP. Mgogoro wa tozo ambao ni wa Tanesco na IPTL  ndio mgogoro uliozaa ESCROW Akaunti, mgogoro wa VIP na Mechmar haukazaa Escrow Akaunti na wala ECSROW haiuhusu. Iweje sasa hukumu ya mgogoro ambao hauhusiani na ESCROW  ndio  iruhusu pesa  kutoka BOT. Ni wazi mahakama haikusema hivo isipokuwa iliposema mali na shughuli zote zikabidhiwe kwa IPTL ilikuwa ikimaanisha shughuli zote ikiwamo na mgogoro wa ESCROW ukabidhiwe kwa IPTL  ili iendelee nao. Ina maana ilikabidhiwa na mgogoro  ambao kuumaliza kwake ili pesa itoke  ni baada ya makubaliano na Tanesco na si baada ya hukumu.Hakuna popote katika hukumu ile paliposemwa hela apewe IPTL isipokuwa ilisemwa Mechmar alikabidhiwe shughuli za IPTL mgogoro ikiwa shughuli mojawapo na si pesa.Si sawa kusema mahakama ilisema pesa apewe IPTL

(  3  ) TANESCO   ILISHINDA   KESI   MAHAKAMA  YA   KIMATAIFA.

Tanesco ilifungua shauri la kulalamikia tozo mahakama  ya biashara ya`kimataifa na ikashinda japo si kwa kiwango ilichokuwa inataka. Kwa maana hii ni kuwa kama Tanesco ilishinda  lakini ikakosa pa kulalamika zaidi kwakuwa mahakama hiyo haina rufaa wala kuomba marejeo(review)  basi hukumu ile ndo ilitakiwa kufuatwa na si vinginevyo.  Na kwa kufuata hukumu ile  Tanesco ingeokoa kiasi cha pesa kwakuwa hukumu hiyo ilipunguza tozo ambayo tanesco walipaswa kulipa kwa IPTL. Kwa kufuata hukumu hiyo Tanesco ingeokoa fedha kuliko hivi  ambavyo fedha zote zimechukuliwa na IPTL. Ajabu ni kuwa hukumu hiyo haizungumzwi na kwanini haikufuatwa pia wahusika wamekaa kimya kama haikuwahi kuwapo.

(  4  ) RAIS   HAKUWA    MKALI    KWA   WAKWEPA  KODI.
Rais amesema kwenye pesa iliyotolewa ESCROW kulikuwa na pesa ya kodi ambayo haikulipwa lakini akasema  hatua walizochukua mpaka sasa ni kuwa TRA wanaendelea kudai kodi hizo. Rais hajasema lolote kuhusu kwanini  kodi haikulipwa tangu awali.  Ameanza kushughulika na hatua ya pili kabla ya hatua ya kwanza.Hatua ya kwanza ni swali la  kwanini walikwepa kodi huku wakijua kuwa kufanya hivyo ni kosa.Tulitarajia kusikia hatua za kijinai. Hatua ya pili ndo ije hiyo sasa ya TRA  kuanza mchakato wa kudai hizo kodi. Huwezi kumdai kodi aliyekwepa kodi kabla hujamchukulia hatua za kutolipa kodi. Ni sawa na mwizi kuiba radio ukaagiza  jeshi la polisi waifuate ile radio kwake halafu iishie hapo.

MWANDISHI  WA   MAKALA   HAYA   NI   MWANASHERIA
0784482959
0714047241

20 comments:

Anonymous said...

Umetoa maelezo mazuri ndugu na ya kweli.Ukweli wa mambo uko wazi kabisa nashindwa kuelewa kwanini viongozi wetu wanakuwa waoga na wanashindwa kuitetea nchi yao kwa nguvu na kwa ukali.Sijui tutafika wapi kimaendeleo kwa hali kama hii.

Anonymous said...

vijimambo acheni kubania ujumbe,tuone koment as long hazina matusi tunaomba mzipublish...kwa sababu viongozi ..wanasoma hizi comments ndio manaa wakija nchi za nje wanatukandamiza na kutwa kutusema tuache kukaa kwenye blogs na kuponda BLOGS,,NO NO NO hatuachi mheshimiwa rais na viongozi wote mnaokujaga huku na kusema tuache hatuachi tutapiga kelele mpaka na nyie msilale WIZI UNAUMA tunapokuja nyumbani kuona viongozi na watoto wao wanaishi vizuri kwa kutofanya chochote wengine hata shuleni tumesoma nao walikua VILAZA TU sasa hivi wazazi wao washawekea mapesa ya wizi wanakula kuku ..lazima hawa watu wawajibishwe ..sisi weneyewe tumesoma vilevile tunahitaji haki itendeke ,,JAMANI HAMNA HURUMA KUONA WATU WANATESEKA USIENDE MBALI DAR ES SALAAM HAPOHAPO HUONI KAMA NI SHIDA ..KWA ASLIMIA YA 97YA WATANZANIA WANA DHIKI YA KUUA?WEE UNAIBA PESA ?SASA Raisi nae anatuchekesha kweli..!!haha eti pesa sio za umma..?yaani kweli sie wajinga kiasi hicho kutuambia watanzaia hivyo..pesa za serikali ni za nani?kama sio UMMA?uongozi ni uongozi na ubinadamu pia ni ubinadamu..!!

Anonymous said...

Kimsingi nakubaliana na mchanganuo alioutoa mwandishi wa makala hii ingawa nitatofautiana naye kidogo katika mchanganuo wake wa kile alichokiita kosa la nne. Si sahihi sana ku-suggest kwamba IPTL walikwepa kulipa kodi tangu mwanzo. Hiyo kodi inayozungumziwa inahusiana na hela hiyo ya escrow ambayo ilikuwa inabishaniwa. Kwa sababu ya dispute iliyokuwepo, kulikuwa na utata wa basis ya kukokotoa kodi ya serikali. Kwa hiyo, kwa wakati huo ilikuwa sawa kwa kodi ya serikali kuendelea kubaki kama sehemu ya pesa hizo zilizokuwa kwenye escrow mpaka hapo dispute itakapotatuliwa na kueleweka IPTL ilikuwa inastahili kulipwa kiasi gani. Baada ya hapo ukokotoaji wa kodi za serikali ungeweza kufanyika na kodi ya serikali kulipwa. Kosa la kutolipwa kwa kodi, if anything, limefanyika baada ya IPTL kupewa hela yote, siyo kabla ya hapo.

Anonymous said...

watanzania wenzangu mkisha kuambiwa Pesa hakuwa ya umma julizeni maanake nini?umma na wakina nani na serikali ina tengenezwa na kina nani mpaka iwe serikali na nchi kama si umma,wanachaguliwa wao na kina nani kama si wana umma.

hakuna kuwajibishwa mtu yeyote hapo change la macho wamekufurahisheni tu nyinyi wana umma mnao foka foka kwenye keyboard zenu kwa sana na mitaani wanakupozeni na mnashangilia mkiona watu wanawajibishwa but in REALITY SI KWELI KWAMBA WANAWAJIBISHWA.subirini tu mtakuja kuniambia.

mmeshatukanwa sana wadanganyika eeeh sana mnaletewa diamond akupozeni roho zenu kwa nyimbo zake na mazaga zaga kibao. ha ha ha.

Anonymous said...

kwa nini mtuhumiwa awe tibaijuka ni yule aliyegawiwa hela na mwizi na jambazi aachwe huru. Muhongo, Rugemalila, Muchwa, SingaSinga,saada mkuya,abraham kinana,professor ,felichism mrababenno ndulu,dr silviaciua likwelile and a bunch of others I wouldn't care to mention. Mbona mheshimiwa kapuliza tu. Kuna kitu gani nyuma ya hili pazia.

Raisi ataendelea kupata kikohozi asichojua kilipoanzia

Anonymous said...

Wakati akijadili suala la escrow naibu waziri mheshimiwa lameck mwigulu alisema mwizi akiiba ukaishia kumfukuza manake unampa likizo ya kwenda kutafuna mabilioni aliyoyaiba, je professor amepata bahati hiyo?

Anonymous said...

Killichonikera ni Kuwa Rais hakuzungumzia yule mwanasheria wa tanesco aliyetumwa kufanya Due Diligence Malaysia kisha wakamtimua,halafu Leo JK anajifanya tunafanya uchunguzi kujua Kama PAP ni mmiliki wa 70% shares za IPTL,what that for

Anonymous said...

Raisi gani anakebehi hela ya nchi yake mwenyewe mbele ya kadamnasi wakati yeye mwenyewe kwa miongo kadhaa amesaidia kuiteremusha thamani mbele ya hizo zisizokuwa za madafu.

HALAFU ANASEMA PESA SI ZA UMMA NI ZA NANI NA ZAO WACHOTE TU? WHAT A SHAME.

MWALIMU NYERERE UKO WAPI BABA YETU UPO WAPI TUNA KU MISS SANA UNGEKUWEPO UCHAFU HUU WOTE WALA USINGETOKEA.

Anonymous said...

Inasikitisha na kufedhehesha jinsi watz tunavyoshikilia bango mambo yasiyo ya msingi na kuyafumbia macho mambo yenye effect na nchi nzima

Anonymous said...



Rais kakubali kwamba kuna utata kwenye umiliki wa 70% shares za IPTL.

Wanafanya uchunguzi kubaini ukweli.

Unabaki kujiuliza, ilikuaje malipo yafanyike kabla ya kuhakiki umiliki halali? Yani uchunguzi unafanyika baada ya malipo kufanyika.

In other words, BoT na ofisi zote zilizoshiriki kwenye huu mchakato wa malipo (pamoja na Ikulu), ziliruhusu malipo yafanyike bila uhakiki wa uhalali wa umiliki wa IPTL.

Only in Tanzania.

Anonymous said...

Rais Kikwete ameseme kuwa pesa ya Tegeta Escrow SIO YA UMMA.
Sasa kwanini AG Jaji Werema alijiuzulu?
Vipi kuhusu kodi ya VAT ambayo haikulipwa kutoka kwenye ile 70% ya Sethi?

Anonymous said...

Watu wanataka kuona mtandao mzima uliofanikisha kuchota pesa kule stanbic unashughulikiwa, sio kiini macho cha Tibaijuka. Hapa sio kwamba Tiba abaki,no ila sio kuishia kwa Tibaijuka na kuanza porojo za kiporo na "mchakato wa uchunguzi" unaendelea. Mbona hakugusia hata kidogo pesa za Stanbic?

Anonymous said...

Tibaijuka hajawajibishwa bali ameombwa kwa unyenyekevu mkubwa ampe nafasi mwenyekiti wa ccm ateue mtu mwingine ktk Club yao ya wizi wa mali ya umma. Jana kikwete hakuongea kama rais bali kama mwenyekiti wa ccm ndio maana ktk ile kamati ya muafaka yeye anamtambua kilango pekee maana ndiye aliyeongoza upande wa ccm. Halafu ndio maana alikuwa anawasema wabunge wa ccm kuwa kwanini hawasemi na sie tulikuwa tunapinga ufisadi, halafu akawa anawaponda wapinzani kuwa wanatafuta cheap popularity. Kwasasa Tanzania haina rais inaongozwa na waziri wa mambo ya nje

Anonymous said...

Kikwete amemdhalilisha sana yule Anna kwa kufurahisha wazee na wanawake wa Daresalaam ,alichokifanya ni aibu ,ila ndio faida ya kuikumbatia CCM ,mtu na elimu yake wamemuingiza kwenye siasa mwisho wake wanampiga na chini tena hadharani na shangwe na vigelegele.

Wasomi ikimbieni ccm hicho si chama cha siasa ,kama una elimu yako na kujibanza huko kwa kufuata ulaghai wa maneno yao ujue utapotezewa ,unaondoka na aibu.Mifano ipo mingi wasomi ndani ya ccm huishia kufukuzwa.

Anonymous said...

Kiukweli mm binafsi nimeshangazwa sana na yaliyokea, Tibaijuka uamuzi umewezekana tena kwa haraka huku akiendelea kuchunguzwa, ila Muhongo yeye baadae, why? Ana u special gani? Na kwa mnaofuatilia TBC na Habari leo mtagundua kulikua na kampeni kubwa sana ya kumtetea kwa nguvu zote huyu jamaa, kuna nini?

Mh.... Nchi yangu Tanzania maajabu hayaishi

Anonymous said...

Nchi hii tilipofikia hata siwaelewi viongozi wa nchi hii bunge lilikubaliana na CAG kuwa katika pesa zilizokuwa kwenye akaunti ya tegeta escrow kulikuwa napesa ya umma ajabu rais anakanusha kuwa haikuwa pesa ya umma sasa kama haikuwa pesa ya umma ilifata nini kwenye akaunti ya escrow kwanini isingepelekwa kwenye akaunti ya IPTL moja kwa moja na kama haikuwa pesa ya umma kwa nini kamfukuza tibaijuka kosa lake ni nini kupewa pesa isiyo ya umma au tatizo ni nini yaani watanzania tunafanywa wajinga tusiojiewa kitu ambacho hakikubaliki mtuhumiwa namba moja anaachwa kwa kuwekwa kipolo na anaadabishwa ambae hakuwa na madhara kwetu.mtu wa kwanza tuliemtaka ni mhongo na sio huyo mama tunataka aliekuwa chanzo cha huyo mama kuzipata hizo hela na sio mpokeaji pasipo mafyongo ya mhongo mama tibaijuka asingepata hizo pesa imenisikitisha sana

Anonymous said...

Mwaka 2010 wafanyakazi walipotaka kugoma JK alisema wakigoma ye ndo mwajiri mkuu na wakigoma watakuwa wamejifukuzisha wenyewe.Sasa kwenye hii ya ESCROW inakuaje anasitasita kuwajibisha wotee na kamtoa kondoo wa kafara tibaijuka peke ambaye yeye amekubali kupoke hizo pesa wenzake wameufyata why kawajibishwa pekee?

Anonymous said...

Kikwete amemdhalilisha sana yule Anna kwa kufurahisha wazee na wanawake wa Daresalaam ,alichokifanya ni aibu ,ila ndio faida ya kuikumbatia CCM ,mtu na elimu yake wamemuingiza kwenye siasa mwisho wake wanampiga na chini tena hadharani na shangwe na vigelegele.

Wasomi ikimbieni ccm hicho si chama cha siasa ,kama una elimu yako na kujibanza huko kwa kufuata ulaghai wa maneno yao ujue utapotezewa ,unaondoka na aibu.Mifano ipo mingi wasomi ndani ya ccm huishia kufukuzwa.

Anonymous said...

Jk na serikali yake (ccm) wameamua kumtafuta mtu wa kuwaondolea nuksi ama wapate cha kuzungumza mbele ya watanzania linapokuja suala la kuwawajibisha mafisadi.
Wakumbuke pia kuwa Tanzania hii siyo ya miaka ile ya TANU, wasitegemee kama watawakamata kwa pumba zisizo na punje za mchele ndani yake.

Anonymous said...

ANGALIYENI JINSI MA CCM WANAVYOO UMBUKA WANAKULANA WENYEWE KWA WENYEWE MAFISADI WAKUBWA TU NA SISI TUMEBAKI KUSHABIKIA UFISADI WAO NA KUWA MASHABIKI WAO WAKATI WAO WANAKULA MAISHA YA RAHA SISI TUPO TUNAPATA MSOTO MOTO MOTO MFYUUUUMWAAA.