ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, December 17, 2014

MSIMU WA SIKUKUU DAR LIVE, WASANII WAELEZEA WALIVYOJIPANGA KUPOROMOSHA BURUDANI KALI

Mfalme wa Muziki wa Taarab nchini, Mzee Yusuf (wa pili kushoto) akielezea kwa wanahabari (hawapo pichani) alivyojipanga kuanguasha shoo ya nguvu katika Tamasha la Wafalme Sikukuu ya Xmas Dar Live. 
Meneja wa Mashauzi Classic, Ismail Rashid 'Suma Ragar' akiongea na wanahabari (hawapo pichani) jinsi walivyojipanga kutoa burudani katika msimu wa Xmas Dar Live wakati wa mkutano na wanahabari hao uliofanyika leo kwenye Hoteli ya The Atriums iliyopo Sinza-Afrikasana jijini Dar . Kushoto ni Mratibu wa tamasha hilo, Benjamin Mwanambuu, Mkurugenzi Bendi ya Extra Bongo, Ali Choki (wa pili kushoto), Mzee Yusuf (wa pili kulia) na Damian Raphael 'MC Dalada Kikombe' kutoka Kundi la Masai Worriors (wa kw nza kulia).
Damian Raphael 'MC Dalada Kikombe' kutoka Kundi la Masai Worriors (katikati) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu makamuzi watakayoyafanya Dar Live katika msimu huu wa sikukuu.

KAMPUNI ya Dar Live kwa mara nyingine imetoa ratiba kamili ya burudani katika msimu huu wa kufungia mwaka 2014 na kuukaribisha mwaka 2015.
Usiku wa Wafalme
Kwa mara nyingine shoo bab’kubwa ambayo ni habari ya mjini kwa sasa ijulikanayo kama Usiku wa Wafalme itagongwa ndani ya ukumbi huo pekee kwa burudani, Desemba 25 ‘Sikukuu ya Krismasi’ ambapo mkali wa muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ atagonga nyimbo zake zote kali siku hiyo.
Diamond ambaye ni mshindi wa tuzo tatu kutoka Channel O zijulikanazo kama Channel O Africa Music Video Awards (CHOAMVA), siku hiyo atatinga na tuzo zake zote hizo ikiwa ni kuwapa shukrani mashabiki wake wote kwa sapoti waliyoitoa huku akipiga nao picha kwenye ‘red carpet’ na kuongea nao mawili-matatu.

Mashabiki pia watapata nafasi ya kumshuhudia Diamond kwa mara ya kwanza akipiga nyimbo zaidi ya 20 jukwaani pasipo kusimama huku akiwatambulisha madensa wapya sambamba na kupiga pia na nyimbo zake zote ambazo zilishawahi kuachiwa na hazijawahi kuisha mpaka mwisho.
Kwa upande wa muziki wa Pwani, usiku huo utafunikwa pia na Mfalme Mzee Yusuf ambaye siku hiyo ataungana na kundi lake la Jahazi Modern Taarab katika kuwaonjesha mashabiki ngoma zao zote zilizopo katika albamu yao mpya ya Chozi la Mama huku wakifunga mwaka na ngoma ambayo ni habari nyingine kwa sasa ya Mahaba Niue.
Mashabiki watakaofika usiku huo pia watapata bahati ya kushuhudia mshindi wa shindano la kumtafuta mwanaume mwenye mvuto kutoka Gazeti la Ijumaa lijulikanalo kama Ijumaa Sexiest Bachelor ambapo mpaka sasa wamebaki washiriki watatu, Yusuph Mlela, Diamond Platnumz pamoja na Ali Kiba.
Mapema kuanzia asubuhi hadi jioni kutakuwa na burudani kwa watoto ambapo watoto wote watakaofika watapata bahati ya kucheza michezo kibao kama vile kubembea, kuteleza, kuogelea na mingine mingi huku kundi la sarakasi la Masai Worriors likiwapagawisha kwa kutoa michezo kibao ya sarakasi , mazingaombwe sambamba na kumwaga zawadi kwa kila mtoto.

No comments: