Advertisements

Thursday, December 18, 2014

OFISI YA MAKAMU WA RAIS YAANDAA SEMINA YA MABADILIKO WA TABIA NCHI KWA WADAU

Sehemu ya Washiriki wa semina ya mabadiliko ya Tabia Nchi inayofanyika mjini Morogoro. Semina hiyo imeandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais
Mgeni Rasmi ambaye ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais,Bwana Sazi Salula akifungua semina hiyo ya mabadiliko ya tabia Nchi.
Mtoa mada katika semina hiyo ya mabadiliko ya tabia nchi Dkt. Yohanna Shaghude akiwasilisha mada kwa Washiriki waliohudhuria semina hiyo
Mgeni Rasmi ambaye ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bwana Sazi Salula akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa semina hiyo ya mabadiliko ya tabia nchi iliyofanyika mjini Morogoro.

Wito umetolewa kwa kila Mwananchi kushiriki katika utekelezaji wa mkakati wa tabianchi ili kuweza kupata maendelo endelevu. Pia kuhakikisha utunzaji wa mazingira unapewa kipaumbele. Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Sazi Salula wakati wa ufunguzi wa semina ya mabadiliko ya tabianchi iliyofanyika mjini Morogoro.

Aliongeza kuwa semina hiyo itaongeza uelewa kuhusu juhudi zinazohitajika katika kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi katika jamii za maeneo ya Pwani. “Mabadiliko ya tabianchi kwa siku zijazo yanaweza kusababisha gharama kubwa za kiuchumi pia kuathiri mamilioni ya maisha ya watu” alisema Bwana Salula.

Akimkaribisha Mgeni Rasmi Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Bwana Julius Ningu amewataka Wadau walioshiriki semina hiyo kuendelea kuongeza nguvu ili kuweza kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi. Alisema kuwa ni jukumu la kila mmoja kusimamia hilo.

Aidha aliwashukuru washiriki kwa kuhudhuria na kuwaomba wakawe mfano kwa wengine katika kutoa elimu ya mabadiliko ya tabianchi ili kuweze kutokomeza janaga hilo.

No comments: