Advertisements

Saturday, December 20, 2014

SAKATA LA ESCROW LAIMALIZA CCM MKOANI IRINGA

Katibu wa chama cha mapAkizungumza na waandishi wa habari amesema kuwa suala hilo linahitaji elimu kubwa kuwaelimisha wananchi kabla ya uchaguzi huo wa serikali za mitaa.induzi mkoani iringa Hassan Mtenga (wa pili kutoka kushoto) akiongoza makatibu wa wilaya kuongea na waandishi wa habari mkoani Iringa (hawapo pichani).


Katibu wa chama cha mapinduzi Hassan Mtenga amekiri kuhusu sakata la fedha za tegeta ESCROW na IPTL kuwa limechangia kudondoka katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika hivi karibuni.
Mtenga amesema dalili za awali kuhusu uchaguzi mkuu utakao fanyika mwakani ni nzuri kukihusu chama na watashinda kwa kishindi kama uchaguzi wa serikali za mitaa.

Aidha amezungumzia kuhusu vijana walioondoka katika chama cha mapinduzi na kujiunga na chadema kuwa umetumika ujanja wa kuwa nunua vijana ili kupigia kura chama cha demokrasia na maendeleo chadema.

Kwa upande wa chama cha mapinduzi wilayani mufindi mkoani iringa mkoani iringa wameulalamikia uongozi wa serikali uliopewa dhamana ya kusimamia zoezi zima la uchaguzi wa serikali za mitaa ambapo dosari nyingi zimejitokeza tofauti na chaguzi zilizopita.


akizungunza na na mtandao huu katibu wa chama hicho wilayani mufindi Miraji Mtaturu amesema kuwa uchaguzi huu umekuwa na changamoto nyingi hivyo kupelekea ucheleshaji wa vifaa pamoja na kufanya uchaguzi kama wa kushitukiza wakati walikuwa wamejipanga toka muda.

Mtaturu ameitaka serikali iangalie kwa makini suala hili la uchaguzi kwa kuwa kuna wananchi wengi wamekosa haki yao ya msingi kwa kuwa walishindwa kupiga kuwa kutokana na kukosekana kwa karatasi za kupigia kura.

Aidha Mtaturu amewapongeza wananchi wa wilaya ya mufindi kuendelea kukipigia kura qwagombea wao na kuwapa ushindi wa asilimia 99 na kuwaachia wapinzania asilimia moja tu licha ya changamoto zilizojitokeza kwenye uchaguzi huo.
(HABARI: FREDY MGUNDA,IRINGA)

1 comment:

Anonymous said...

Hapa hata tukikaa vikao mia mbili bado ukweli unabaki pale pale viongozi wetu wa CCM na serikali nzima imetufikisha hapa tulipo! Kuna mambo mengi saana ambayo nikiwa mmoja wa walioko karibu saana na viongozi wetu hawasemi ukweli tumekuwa tukidanganyana kila siku. Namsifu saana mama Maria NYERERE kwa kusema ukweli ndani ya chama chetu kuna mambo yasiyoitakia mema Tanzania!! kuanzia ngazi ya juu hadi balozi wa nyumba kumi!! Wakati umefika wa kubadili dira na mwelekeo ndugu zanguni wa Tanzania..