Advertisements

Thursday, December 18, 2014

TIBAIJUKA ASEMA HAWEZI KUJIUZULU


Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Tibaijuka akizungumza na waandishi wa habari kwenye hotel ya Hyatt Regency Dar Es Salaam, The Kilimanjaro  
.
Dar es Salaam,
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Profesa Anna Tibaijuka,amekutana na waandishi wa habari na kuzungumzia sakata la Akaunti ya Escrow,huku akisema haoni sababu ya yeye kujiuzulu kutokana na kudaiwa kuhusika katika sakata hilo.

 Alisema hawezi kufikia uamuzi wa kujiuzulu kwa kuwa hana kosa kwani hajatajwa mahala popote katika ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali ( CAG ),ingawa hakupewa nafasi ya kujitetea na Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC).

Alisisitiza fedha alizopewa na Rugemalila ni mchango wa Shule ambapo alisema lengo lake kuwasaidia watoto wa kike kupata elimu bora.
 Alipoulizwa kuhusu kujiuzulu  alisema hawezi jiuzulu kwani haoni sababu ya yeye kujiuzulu.

14 comments:

Anonymous said...

Mama jiuzulu tu. Menzako Lowassa alijiuzulu hata kama hakutajwa kuiba pesa.

Marekani hata kama waziri hakuhusika na wizara yake ina matatizo au kapokea mchang bila ya yeye kujua ulikuwa sehemu ya scandal, huwa anajiuzulu.

Kubali mama yaishe. Wewe ni kiongozi makini, kubali kuwa huyafahamu haya ila kutokana na scandal yenyewe hata kama ulikuwa na nia nzuri, kubali yaishe.

Anonymous said...

wee Mama acha ubabaishaji YOUR TO EDUCATED NAKUONGELEA JAMBO KNOWING KUNA SOME KIND YA VITU HAVIELEWEKI..mchango wa shule,MUOGOPE mungu MASKINI WANAHITAJI MAISHA YA AFADHALI PIA..TUNAJUA HAPA WANAWEKA MIKAKATI YA KUFUNIKA KUBANDUA..IPO SIKU YENU INAKUJA MUNGU HALALI..yamemkuta Ghadaff bwana..!

Anonymous said...

Acha ujanja wewe Profesa, ulimegewa na ulifikiri watu hawatajua. Thanks to Kafulila. You have to go and go before it gets worse, now we are told your daughter also had a share.

Maskini hawana dawa wala chakula, nyie mnagawana kodi zetu. This is a big scandal. you have to go and go now!

Anonymous said...

Mama profesa, are you serious?

Anonymous said...

Kujiuzulu ni kuondoka kwa heshima au sivyo utafukuzwa.

Anonymous said...

Ndiyo maana anaitwa Professor, uongo mtupu hup!

Anonymous said...

Ndio maana waliipinga rasimu ya Warioba ambayo ilikuwa na maadili ya viongozi. Maadili yote wakayaondoa.

Anonymous said...

HIVI HUYU MAMA ANAMUME AU HANA? SI AJIULIZE KWAMBA KAJISAIDIA KICHAKANI AU CHOONI? KAMA HAJUI TOFAUTI YA CHOO NA KICHAKA HUYO SI PROFESA WA KWELI....

Anonymous said...

mnatowa comment humu wanazipata hao wakuu halafu wao wanaangalia upepo wenu ukoje,hakuna atakaye jiuzulu because salaka hili kubwa lina aanza toka juu mpaka kwenye sina so na wajuu nao wajiuzulu.

dawa kuingoa ccm.wanabebana wanafichana wanasaidiana wanakwiba wote. ndo mmaana mtu hataki kujiuzulu.

only in Tanzania uzo huu wote unatokea.

na mdau hapo juu usileta zako za kuleta lowassa alilazimishwa ajiiuzulu haku tahari kujiuzulu mwenyewe na yeye mwenyewa alihusiku

hata zako unachota kwake utakula kwake mwako huu.

Anonymous said...

Hajiuzuru mtu hapa. Imeeleweka kwamba kaka JR amemueleza dada yake kuwa mgao huo sio yeye peke yake aliyefaidika. Wakubwa wengi walipata pia na kampa orodha. Baada ya kuipitia hiyo orodha hasa ile ya stanbic na ile ya cash prof. akastuka. Hiyo ndio hasa sababu ya jeuri. Hajiuzuru mtu mpaka kieleweke kwa wote. Mbona mambo bado mabichiiii!!!

Anonymous said...

Tatizo umeshiriki haijalishi unaitumiaje hiyo fedha. Aibuuuu

Anonymous said...

Sisi wabongo bana tunakurupuka tu, tumewasahau Wizara ya fedha. Wizara ya Fedha wao ndio wahusika wakuu katika hili.

Anonymous said...

mtanivumilia wahusika.
kweli ni mchapa kazi lakini si muadilifu kama walivyo wengi wakuu wa ccm.

Asepe tu,au akisanzue au aishie tu

kuanzia leo nawaweka wahaya kwenye number 2 ya wezi wakuu wa nchi hii. na nafasi ya 3 inashikiliwa na wakurya. mwizi number 1 anajulikana. wakipata madaraka ya umma wanafikiria kuiba tu. nothing else. they are good in nothing.
lengo wajirekebishe.
kuanzia leo popote ninapowaona najua nimekutana ni mwizi.

Anonymous said...

HAYA MZEE WA MIAKA 70 KAKATA MTI JELA MIEZI SITA, WIZI WA MABILIONI WANATAMBA

KAZI IPO KWELI KWELI