ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, December 23, 2014

TIBAIJUKA: KWAKUWA RAIS AMETENGUA UTEUZI WANGU, SASA NIPO JIMBONI NATATUA KERO ZA WANANCHI

Wananchi mkoani kagera wamepinga uamuzi wa Rais wa jamuhuri ya muungano wa tanzania Dk Jakaya Mrisho Kikwete kwa kumuondoa madarakani waziri wa ardhi nyumba na makazi na kuwaweka kiporo viongozi wengine walioshiri kuhujumu pesa za akaunti ya Tegeta Escrow.
Wakiongea na ITV wananchi wa mkoa huo wamesema hawajajua nini hatima ya Rais wa jamuhuri ya muungano wa tanzania Dk. kikwete kwa kuwaweka Kiporo mawaziri wengine waliohusika katika sakata hilo na kumuuondoa waziri Tibaijuka napia wamebaki na sintofahamu ambapo wamemtaka Rais kutoa ufafanuzi kuwa licha kumg’oa madarakani kiongozi huyo Je, Pesa hizo zitarudishwa kwenye akauti hiyo ya TEGETA ESCROW au la.


Nao baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa vya mkoa huo akiwemo katibu wa siasa na uenezi wa chama cha mapinduzi mkoa wa kagera Hamimu Mahamudu amepongeza uamuzi wa Rais alioutoa jana wakati akiongea na wazee wa jijini Dar es salaam kwa kumuondoa kiongozi huyo huku katibu wa chama cha Demokrasia na maendeleo chadema katika manispaa ya Bukoba Victor Sherejei akisema kuwa Rais hajatoa uamuzi sahii ambapo amemtaka Rais kuwafahamisha watanzinia kuwa Pesa za Escrow zitarudishwa lini katika akanti hiyo au kuwaondoa viongozi hao madarakani ndio suluhisho la kwamba pesa hizo hazirudishi?.


Kwa upande wake aliyekuwa Waziri wa ardhi nyumba na makazi Profesa anna tibaijuka amesema licha Rais kumuondo katika nafasi yake aliyokuwa nayo sasa amerudi jimboni kwake kwaajili ya kutatua kero na changamoto mbalimbali za wananchi wake kwani nafasi aliyokuwanayo ilikuwa haimpi nafisi ya kuwasimamia wananchi katika jimbo lake na kwamba Pesa hizo alipewa na lugemalila zilikuwa za kusaidia shule na alipewa kama zawadi bila kujua kama pesa hizo zilitoka katika akaunti ya TEGETA SCROW ndomaana hakutaka kujiuzulu mapema.


Chanzo:ITV

11 comments:

Anonymous said...

its so funny ulivyokuwa serikalini hujaona wajibu wako kutatua kero za watu wako wa jimboni sasa huna kibarua ndo unakwenda kwa watu wako jimbono. kazi kweli kweli.

lakin nakupa pole sana mama kwa sababu wamekufanya wewe kondoo wa kafaraa na wengine wanaachiliwa tuu.pole sana mamaa

Anonymous said...

Of all the people wadau waosha vinywa na wavimba macho wanaoonekana kuwa na upevu walau kidogo kushindwa kuchambua issues.

Kuna mambo mengi ya kutia shaka....watu hatuhoji


Kwa nini kikwete anasimamia maslahi ya IPTL badala ya TANESCO ...Watu hatujiulizi

Kwa nini ameongea kwa kubeza sana kwamba pesa zimebebwa kwa magunia

Kwa nini ame ignore ishu za stanbic

Nini kitafanyika kuhusu Mkataba wa IPTL ,,,Bado kimya

Halafu mapoyoyo ya vijimambo JF yanashangilia Tiba kuondolewa just because yeye amejulikana kachukua pesa

Nani waliochukua mapesa mengine...thats non of our business

Najuta kuwa mtanzania...deep from my heart

Anonymous said...

masikini mama tibaijuka,kukili kwake kumemweka msalabani.
Any way njoo nyumbani bukoba tuanze miradi ya kuweka senene katika makopo na pombe la lubisi

Anonymous said...

Kweli ni vyema sasa atatue kero za wananchi baada ya kero zake binafsi kututatuliwa na kaka JR!!!

Anonymous said...

ushomile ndo umekupomza mama pole sana

Anonymous said...

Kikwete amemdhalilisha sana yule Anna kwa kufurahisha wazee na wanawake wa Daresalaam ,alichokifanya ni aibu ,ila ndio faida ya kuikumbatia CCM ,mtu na elimu yake wamemuingiza kwenye siasa mwisho wake wanampiga na chini tena hadharani na shangwe na vigelegele.

Wasomi ikimbieni ccm hicho si chama cha siasa ,kama una elimu yako na kujibanza huko kwa kufuata ulaghai wa maneno yao ujue utapotezewa ,unaondoka na aibu.Mifano ipo mingi wasomi ndani ya ccm huishia kufukuzwa.

kwa nini mama usomi wako wote huu umejiingiza kwenye siasa au ndo ushomile wako huu umekuponza.

Anonymous said...

shame on you Tibaijuka, shame on all Tanzanian leaders including the President. All the money should be returned back to the account first before other actions taken against these thugs. Tanzanian leadership is full of thugs and thieves who feel no shame stealing public funds in the day light.God bless Tanzania we have a long way to go, give us strength to root out this kind of filthy leaders. Aluta continua!!

Anonymous said...

anyone in defense of Tibaijuka exhibits the depth of the lack or misunderstanding of ethics in our society. nothing she did or the manner she received the million dollars can be justified.

she can holler and cry and rally the sympathies of her clansmen and women but she will remain utterly wrong.

no minister or government official should receive money from any source without making appropriate declaration.

have you heard of conflict of interests?

what do you think would have been her position when the matter of IPTL was being discussed at the cabinet?!!

Anonymous said...

let me ask you one question big boss at 1:27 do you know the history of IPTL? Who was the minister when this scandal was boiling up?
why only her? Why only ukombozi bank what about stanbic bank and many other more?
think and if you cant do your research and then come here again and comment what you have comment up there with no evidence.
ponder you brain to think BIG AND DEEP DOWN.

Today Tanzanians are not Yesterday or the day before yesterday Tanzanians, we don't take cheap ignorant stuff like this,kuwajibiswa only her.

Anonymous said...

let me ask you one question big boss at 1:27 do you know the history of IPTL? Who was the minister when this scandal was boiling up?
why only her? Why only ukombozi bank what about stanbic bank and many other more?
think and if you cant do your research and then come here again and comment what you have comment up there with no evidence.
ponder you brain to think BIG AND DEEP DOWN.

Today Tanzanians are not Yesterday or the day before yesterday Tanzanians, we don't take cheap ignorant stuff like this,kuwajibiswa only her.

Anonymous said...

Nionavyo mimi Tanzania tunakazi kubwa sana ya kubadisha maadili na hulka zetu za kijinga, uchafu wetu haupo kwa viongozi tu upo pia from our grass roots.

Tunaishia kuwalaumu viongozi kila dakika wakati sisi ndio tunaowachagua ili walinde maslahi yetu madogo madogo.

Tunapata mshahara laki na nusu, familia watoto wa tano, vimada wawili na watoto kadhaa wengine. Kila siku vikao vya kila siku kwenye baa, zungusha kwa saanaaaa. Hizo pesa tunazitoa wapi budget ya karibu mil 2 kila mwezi na sisi ni wafanyakazi wa kawaida?

ofcourse lazima tumchague mtu anaye kula matawi ya juu wakati huo huo atuachie na sisi tule matawi ya chini.

Culture hii ya mtanzania wa kawaida haijaanza leo, ndo maana wabongo hatuandamani hata tukikandamizwa vipi, what for?