ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, January 28, 2015

KINANA AZUNGUMUZA NA WAJUMBE WA HALMASHAURI KUU YA CCM WILAYA YA CHAKE CHAKE PEMBA

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM wilaya ya Chake Chake Pemba ambapo aliwataka viongozi wa CCM kutenda haki, kujipanga na kuchagua viongozi wanaokubalika.
Mkuu wa mkoa wa Kusini Pemba Mwanajuma Majid Abdala akisalimia wananchi wa Mchangani, ambapo Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alifika kushiriki ujenzi wa tawi la CCM.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (kulia) akishiriki ujenzi wa ofisi ya Tawi la CCM Mchangani,kushoto aliyebeba tofali ni MNEC wa Chake Chake Daudi Ismaili akisaidia ujenzi, Katibu Mkuu yupo kwenye ziara ya kujenga, kuhamasisha na kuimarisha Chama Cha Mapinduzi,Pemba.
Vijana wawili kutoka vyama vya upinzani kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Chadema Uwandani Chake Chake Pemba Kombo Ali Abdala na Kulia ni Mwenyekiti wa ADC Uwandani Mohamed Said Abdalla wakishiriki ujenzi wa darasa pamoja na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
Vijana wawili kutoka vyama vya upinzani kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Chadema Uwandani Chake Chake Pemba Kombo Ali Abdala na Kushoto ni Mwenyekiti wa ADC Uwandani Mohamed Said Abdalla wakiongozana na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana baada ya kumaliza kushiriki ujenzi wa madarasa katika skuli ya Uwandani Pemba.
 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozana na viongozi na wananchi kuelekea Kilindi Pemba kuona maendeleo ya kikundi cha kutunza mazingira cha Hatugombani pamoja na kushiriki kupanda miti ,Pemba.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Hadija Abood akishiriki kupanda mti wa mkungu wakati walipotembelea kikundi cha kutunza mazingira cha Hatugombani.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Chake Chake Pemba ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa na utamaduni wa kuuliza maswali kwa viongozi wao hasa wabunge na wawakilishi wanapokuja kuwahutubia kwani wamekuwa wakipoteza muda mwingi kuwahutubia wananchi hao kuhusu CCM badala ya kuzungumzia namna wanavyoshughulikia changamoto za wananchi kwenye majimbo yao.
Wananchi wa Chake Chake pemba wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipohutubia kwenye viwanja vya Pujini Kunvini, mkoa wa Kusini Pemba.
Kijana Said Abdalla Ibrahim akionyesha kadi yake ya CUF ambayo ameamua kuirudisha na kujiunga na CCM mbele ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Pujini Kunvini,Chake Chake Pemba
Kijana Said Abdalla Ibrahim akionyesha kadi yake ya CUF mbele ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwenye mkutano wa hadhara Chake Chake Pemba.
 :
Kijana Ghalib Bedui Khamis akionyesha kadi yake ya CUF kabla ya kumkabidhi Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na kujiunga na CCM kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Pujini Kunvini,Chake Chake Pemba.
Kijana Ghalib Bedui Khamis akitangaza kujiunga na CCM kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Pujini Kunvini,Chake Chake Pemba.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar) Vuai Ali Vuai akihutubia wakazi waliohudhuria mkutano wa hadhara na kuwaambia CUF wanaanza kukiuka makubaliano ya MUAFAKA na kutaka CUF kuheshimu makubaliano hayo.
Wananchi wakisikiliza mkutano kwa makini.
Shadia Mohamed Mwakilishi wa Chake Chake Pemba akihutubia kwenye mkutano uliofanyika Pujini Kunvini ,Pemba.
Mbunge wa Viti Maalum Asha Omar akihutubia wananchi waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa hadahara uliofanyika Pujini Kunvini na kuwaambia vijana waache kutumika na watu wasiokuwa na manufaa kwao.
Mbunge wa Viti Maalum Faida Bakari akihutubia wakazi wa Chake Chake Pemba na kuwaambia masuala yanayohusu ardhi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Pujini Kunvini.
Mwakilishi wa Kuteuliwa na waziri wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi,Vijana na Wanawake akihutubia wananchi waliohudhuria mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahma Kinana na kuwataka wananchi hao hasa wanawake kuisoma kwa makini Katiba mpya iliyopendekezwa


No comments: