Zainab Buzohera Enzi ya Uhai Wake.
Sekunde dakika masaa siku wiki miezi imepita na leo ni mwaka tangu ulipoitwa na Mwenyezi Mungu (S.W.T). na kutuachia uchungu usioelezeka . Pengo ulilotuachia haliwezi kuzibika bali tunamshukuru Mungu kwani kazi yake haina makosa. Tunaendelea kumuomba akupumzishe kwa amani hadi hapo tutakapo kutana kwani sisi wote ni wapitaji.unakumbukwa na baba mzee Haroun mama Bi Rehema wadogo zako ndugu jamaa marafiki na wote waliokufahamu .unakumbukwa sana kwa ucheshi wako moyo wako wa utoaji na ushirikiano na wengi . Mwenyezi Mungu akupumzishe kwa amani na aendelee kutufariji . Sisi wote ni wake na kwake tutarejea.Inna lillah wa inna lillah rajiun
No comments:
Post a Comment