Advertisements

Monday, January 19, 2015

Mh. January Makamba, Urais Sio Sawa na Kucheza Filamu

Wanajamvini,Nawasalimu.
Nimelazimika kuanza na hiyo kauli hapo juu kutokana na unyeti wa habari yenyewe.
Nitakuwa namwendelezo wa kutoa ufafanuzi wa mambo mbalimbali yanayoikabili Tanzaniakwa kutumia mifano hai na kumbukumbu rasmi zilizopo Tanzania.
“Ni bora Simba wakali mia moja walioko Nje kuliko nyoka mdogo mmoja aliye ndani [“Godbless JonathanLema]. Haya maneno aliwahi kuyatoa Mbunge Lema, nayafananisha na kijitabualichokitoa Mh. January Makamba. Namheshimu sana [ Hata yeye anajua hilo!]lakini sina budi kusimamia ukweli na kukemea pale inapobidi!. Tanzania hii iliwahi kupata viongozi vijana wengi tu lakini historia inaonyesha waliwahi kuligarimu Taifa kutokana na ufinyu wa kufikiri na uharaka usiokuwa na tija!.Mfano Mh Raisi Kikwete, ndiye anaonekana kuwa Raisi kijana kuliko wote waliopata nafasi hiyo kwa siku za usoni lakini makubwa aliyoifanyia taifa hakuna ? aliwahi kuwa Waziri akiwa na miaka 38 tu?. Hivyo Umri sio kigezo cha kutushawishi kukupa uongozi. Uraisi sio sawa na kucheza filamu?.

Pili, Vijana tulio wengi hatuitaki ccm, yaani tunayavumilia sana majani hata hiyo rangi tungeiteketeza kabisa!!!!. Ukiona kijana yupo ccm jua lazima anapata mnofu? Vinginevyo hakuna au Baba yake aliwahi kuhudumiwa naccm hivyo na yeye anatega mpira?. Kutokana na sababu hii makini kabisa tunakuomba sana tena sana [Nakuheshimu sana Mkuu, hata wewe unajua hilo]usituharibie sifa ya ujana wetu kwa kutaka Makuu wakati bado unastahili kuwa nasubra baadae kama wataka nafasi hiyo ukaipata [ila kupitia chama kingine Mkuu].Kutunga kitabu kinachoelezea kuhusu Tanzania mpya ni maneno tu ambayo kwamtazamo wangu hayana uhalisia wowote ule.

Tatu,Nimewahi kuona watu wengi sana hasa walioko ndani yaccm wakikana maandiko yao yaliowahi kuwapa PHD, mfano DR. Harrison Mwakembe aliwahi kuzungumzia muungano wa serikali tatu kwenye kitabu chake lakini baadaye kupata tu ubunge hatimaye uwaziri kwenye uhalisia akaja kukana maandiko yake mwenyewe hivyo na hii Tanzania mpya ulioitazamia pindi utakapo pata nafasi basi itakuwa hivyo hivyo Mkuu , nakushauri egemea kwenye nini umewahi kuwafanyiaWatanzania na imebaki kama historia nasio utawafanyia nini tukikupa nafasi [uzoefu ni lulu Mkuu popote pale Duniani].Mh Nasari aliwahi kusema nanukuu ‘’CCMNI KAMA UKOO WA PANYA,BABA MWIZI MTOTO MWIZI’’ [Ukikasirika niombee].
Mwisho, Tanzania inahitaji kikongozi mwenye hofu ya Mungu [yaani mwenye hata kahistoria ka kuwa shehe,padre au hata mchungaji jamani] kutokana na sababu kuu moja kuwa Tanzania ni nchi pekee Duniani ambayo haina ‘’NationalPolicy’’ mtu akipata nafasi ya uwaziri tu anaweza kusema futa somo lahesabu kwa shule za msingi watasoma wakiwa sekondari kisa mwanae halipendi au kwasababu tu ya uswahiba na rafiki yako unaamua tu kuanzia kesho wewe utakuwa Mkuu wa wilaya [ kwa mfano tu wadau huyo jamaa alikuwa muuza chipsi leo anapata zali la kuwa mkuu wa wilaya]. Tunataka kiongozi mwenye hofu ya Mungu ili tutengeneze hizo policy kwanza maana nchi ipo pabaya.
Ila kiukweli nakupongeza kwa kutangaza nia na sio kwa kutoa kitabu, tuachie tukupime nini aulichowahi kuifanyi taifa hili Mkuu. Niombee kwa aliyekasirika. Nawatakia sikunjema
By 
Elineema J Mosi
CPA[T]-Arusha,Tanzania.

5 comments:

Anonymous said...

Kijana Eliakeema unanishangaza kidogo. Mimi siyo mpiga debe wa Makamba, lakini unamlaumu kwamba hajafanya lolote jema kwa Taifa. Jee? hao thugs uliowataja (Lema na Nasari) wamefanya nini la maana Kitaifa? Eti wewe na vijana gani?hamuitaki CCM? Oooh, unatoka Kilimanjaro/Arusha, the hotbed of Chadema lunatics? Let's be frank, the sole purpose of Chadema is to install a Chagga president! Unfortunately, the odds are not in their favor. So, to make Itself relevant Chadema has no other choice except to keep on, instilling fear and label the ruling party as the Enemy. Strategically, that will not work simply, because Chadema has proven to be an incapable and power hungry party which has done nothing positive to our beloved nation. Sorry Mosi na vijana wote wa chadema!

Anonymous said...

Una ushamba bado au elimu ndogo

Anonymous said...

Unajua hapa ndio utajua kwa nini shule za Tanzania ni sifuri, huyu aliandika hapa kasoma, sasa asiyesoma anaandika nini? Lema unamtumia kama mfano? Kufananisha Lema na mtu yoyote ni wastage.

January anaweza kuwa hana vigezo vya uongozi, lakini sio kutokana na factors zako hapo juu.

Anonymous said...

Mimi siyo Chadema na pia siyo CCM..lakini kama kijana mwenzenu ninaunga mkono maoni ya muandishi kwa upeo wangu..kama wewe ni kijana kutoka Tanzania ambae umezaliwa na kukua chini ya utawala wa CCM basi utakubali kuwa mabadiliko ni lazima nchini mwetu!! CCM siyo Mungu mtu kuwa ndiyo chama pekee kitakacho tufikisha kileleni...kama kijana makini basi angalia history utakuta popote duniani mabadiliko yanaletwa na ubadilishaji wa watawala..kamwe tusiote kuwa tukibadilisha sura za uongozi ndani ya CCM tutafika !! si nchi tajiri wala masikini wote wanabadilisha watawala..Lema na Nassari ni vijana wenzetu tunapaswa kuunga mkono juhudi za kijana yeyote anaepambana nje ya CCM siyo ndani ya CCM!! Nani hafahamu shida wanazozipata vijana wa upinzani Tanzania? Lema na Nassari hawashindwi kuingia CCM lakini wamechagua njia mbadala ..Januari ni kijana mwenzetu pia na anao uwezo wa kuongoza lakini yupo ndani ya CCM!! hawezi kuja na mapya..atazungukwa na sura zilezil e za kulindana na kuoneana aibu kama ambavyo wote tunaona kinachoendelea kwa sasa!! CCM imelewa inahitaji kuwekwa kando !!ni kawaida kwa watawala kulewa wanapokuwa madarakani kwa muda mrefu ni asili ya binadamu..kwa hiyo kama kweli sisi vijana tuna nia ya dhati ya kuikomboa Tanzania yetu hatuna budi kuachana na CCM !!

Anonymous said...

Inaonekana una shida ya kufikiri, wenzako wote wameandika lugha ya kiswahili, kwenye blog ya kiswahili. Wewe unaandika kiingereza mahali pasipotakiwa na unachanganya changanya ovyo. Inaonekana hujiamini na unachokiafanya au ulikuwa umelewa wakati unaandika....Nataka nikuambie kuwa hata kama CCM itashinda haitashinda kama ilivyozoea hata kama wataiba kura kama walivyozoea kufanya. Watanzania wa leo wameamka, siyo wale wa kushangilia CCM!CCM! Tumechoka na ufisadi na wizi unaofanywa huko serikalini.....kwa kifupi tunachokitaka ni mabadiliko wenye utendaji kazi mzuri na wenye tija na siyo vinginevyo kitu ambacho kwa bahati mbaya ndani ya CCM hakipo. Acha kukashifu watu binafsi (individuals) kwani kufanya hivyo unazidi kuonyesha ujinga wako na kuonekana juha.