ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, January 3, 2015

Mtuhumiwa wa ujambazi na mauaji auawa na wananchi

Kamanda wa Polisi Tarime Rorya, Lazaro Mambosasa

Mkazi wa kitongoji cha Nyahongo kilichoko kijiji cha Nyarwana wilayani Tarime mkoani Mara aliyekuwa akisakwa na polisi kwa tuhuma za ujambazi na mauaji ameuawa na wananchi katika shambulizi ambalo lililojeruhi wanakijiji watatu.

Wambura Kihongwe (40) ameuawa na wananchi kwa kukatwa mapanga kichwani na sehemu mbalimbali za mwili huku naye akiwajeruhi watu watatu waliojaribu kumkamata ili afikishwe kwenye vyombo vya sheria.

Kamanda wa Polisi Tarime Rorya, Lazaro Mambosasa alisema kuwa" tukio hilo la kuuawa kwa mtuhumiwa huyo aliyekuwa anasakwa kwa muda mrefu na polisi bila mafanikio lilitokea juzi wakati wananchi walojihami kwa silaha za jadi kutaka kumkamata walipopambana naye akiwa anatumia panga alilokuwa amelificha kwenye koti na kuanza kuwashambulia ili kuwatoroka.

Kamanda Mambosasa alisema katika harakati za kupambana na mtuhumiwa huyo aliwakata na kuwajeruhi kwa pangaMasebo Nyamaruri (30) na Julius Chacha ( 20) aliowakata mkono kila mmoja na Thomas Masama ( 32) aliyepigwa panga kichwani na kwamba wanashikiliwa na polisi.

Wakati huo huo, mkazi wa kitongoji cha Nchoke Mosoma Marwa Robogo(23) amechomwa kisu na kuuawa na mtuhumiwa Kihengu Nyambaha(50) kwa madai ya kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mpenzi wa Robogo (jina linahifadhiwa).

Kamanda Mambosasa alisema aliawa siku ya mwaka mpya na muuaji alitoroka na huenda amekimbilia Kenya ama mikoa mingine jirani na kuwataka wananchi kusaidia polisi kumkamata mtuhumiwa ili kufikishwa katika vyombo vya sheria.
CHANZO: NIPASHE

No comments: