ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, January 7, 2015

SERIKALI YATAKIWA KUKOMESHA UBABE KWENYE UKEKETAJI

DSC_0300
Mratibu wa kituo cha TFGM na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Mtakatifu Catherine Laboure ya Kijiji cha Masanga kilichopo wilayani Tarime mkoani Mara, Thomas Maruga akiwatembeza maeneo mbalimbali ya shule hiyo na Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kulia) na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA), Dkt. Natalia Kanem (kushoto) wakati wa sherehe ya mahafali ya sita ya mabinti waliokwepeshwa msimu wa ukeketaji (Waiseke wa Kisasa).(Picha za Zainul Mzige wa MOblog).
Na Mwandishi wetu, Tarime-Mara
SERIKALI imeombwa kuhakikisha inakomesha ubabe unaotumika kukeketa mabinti wa koo za Kikuria nchini.
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Kituo cha kupambana na ukeketaji cha Masanga, Tarime Sista Germaine Baibika akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukamilika kwa sherehe ya mahafali ya sita ya mabinti waliokwepeshwa msimu wa ukeketaji.
Alisema jumla ya mabinti 634 wamehitimu mafunzo ya miezi miwili yanayogusa haki za binadamu, haki zao, masuala ya afya na kuzitambua na kuezinzi mila nzuri.
Aidha wamejifunza kazi za sanaa na usanii.
Alisema adha kubwa wanayokumbana nayo mabinti hao waliotoka katika kituo hicho ni kukamatwa kwa nguvu na kupitishwa kisu cha Ngariba bila wao wenyewe kuafiki kwa dai la kuendeleza mila.
“Hii sio mila” anasema sista Germaine na kuongeza kuwa hakuna mila inayotengenezwa kunyanyasa watu wengine au kulazimisha mambo yasiyofaa katika jamii, mila hiyo ikiwepo lazima ipigwe vita.
DSC_0480
Mgeni rasmi Waziri wa Kazi na Ajira, Mh. Gaudentia Kabaka (wa pili kushoto) akiwasili kwenye mahafali hayo pamoja na Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kushoto) aliyeambatana na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA), Dkt Natalia Kanem.
Alisema serikali isiache kuwatetea mabinti hao kwa dai la kuwa hiyo ni mila kwa kuwa wanaofanyiwa vitendo hivyo hulazimishwa na haifanyiki kwa ridhaa yao.
Alisema wapo mabinti walioletwa na wazazi wao kuepushwa na janga hilo, wapo waliotoroka kwa wazazi wao na wapo walioletwa katika kituo hicho na polisi kutoka makwao.
Mafunzo hayo ya mwezi mmoja yamelenga kukabiliana na msimu wa ukeketaji ambao sisita huyo alisema mwaka jana ulianza mapema Novemba na unaendelea hadi mwaka huu wakati kimila mwaka huu si wa ukeketaji.
Kwa mujibu wa mila za Kikuria ukeketaji hufanyika katika mwaka unaogawanyika, mwaka 2015 haugawanyiki.

DSC_0492
Mhashamu Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Musoma Mkoani Mara, Michael Msongazila akiwasili kwenye sherehe za mahafali ya sita ya kituo cha kupambana na ukeketaji Masanga wilayani Tarime mkoani Mara.
Mafunzo hayo ambayo yamelenga kuwatoa mabinti wa kisasa wenye mwelekeo wa maisha yenye hali bora mabinti wanaofika hapo huwa hawataki kukeketwa na ndio maana mwaka huu walipata tatizo la binti mmoja kuzimia wakati alipomuona baba yake katika maeneo ya kituo hicho.
Alisema wapo wazazi wakorofi wanaokuja kudai watoto wao lakini pia ipo jamii korofi inayotumia ubabe baada ya wasichana hao kutoka hapo wanakeketwa kwa lazima.
Katika hafla hiyo iliyoendeshwa na masista wa shirika la Daughters of Charity of St. Vincent De Paul, Waziri wa Kazi na Ajira Mh. Gaudentia Kabaka aliwapongeza wasichana hao na kuwataka kuwa mfano katika jamii na kutekeleza wajibu wao.
Alisema wamekuwa mabinti wa kisasa kwa kukataa ukeketaji na hivyo wao wanastahili kuwa walimu kwa wenzao.
DSC_0433
Maandamano ya wanafunzi wa Shule ya Mtakatifu Catherine Laboure iliyopo kijiji cha Masanga wilayani Tarime, mkoani Mara wakiwa na mabango yenye jumbe mbalimbali za kukemea ukeketeji wakisindikiza dada zao wahitimu wa kituo cha FGMT katika sherehe ya mahafali ya sita ya mabinti (Waiseke wa kisasa) waliokwepeshwa msimu wa ukeketaji yaliyofanyika mwanzoni mwa wiki.
Aidha Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez amewataka mabinti hao kuwa chachu ya mabadiliko katika jamii na kuwa chanzo cha kubadili kizazi kijacho.
Alisema wamesimama madhubuti kupinga mila potofu na uonevu na kusema kwa kitendo chao wamewafanya wengine kuwaiga na kubadilika.
Alisema ukeketaji ni mila potofu na kusema kwa msaada wa shirika la Umoja wa mataifa la Mpango wa familia (UNFPA) na taasisi nyingine zinazopambana na ukeketaji kwa kipindi cha miaka saba wamefanikiwa kuwoakoa wasichana 2001 wasikeketwe.
Aidha mabinti hao wameokolewa dhidi ya ndoa za utotoni, ujauzito wa mapema na kushindwa kuendelea na masomo.
DSC_0425
Naye Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA), Dkt Natalia Kanem amesema ni vyema mapambano dhidi ya ukeketaji yakaendelea kwa kuwa wanaoshabikia ni viongozi wa kimila na ngumu kuiondoa ila kwa juhudi za jamii yenyewe.
Katika sherehe hizo ambapo pia askofu wa Musoma alikuwepo na viongozi wengine wa kiserikali pia Ngariba walioacha kazi hiyo walikuwepo kuelezea ubaya wa mila hiyo.
Suala la ukeketaji ni kitu cha kawaida katika mikoa ya Manyara 71%, Dodoma 64%, Arusha 57%, Singida 51% na Mara 40%.
Viongozi waliopata muda wa kuzungumza walisema kwamba ukeketaji unatakiwa kukomeshwa mara moja kwani ni tatizo si tu kwa jamii bali kwa wale ambao wanafanyiwa kisaikolojia na kitabibu.
DSC_0439
Wahitimu mabinti 37 waliokwepeshwa msimu wa ukeketaji wa kituo cha TFGM cha kijiji cha Masanga wakiwasili na maandamano kwenye sherehe za mahafali ya sita ya kituo hicho.
Moja ya kazi inayoifanywa na kituo cha Masanga ni ushauri wa kisaikolojia kutokana na wasichana wengi kufika hapo wakiwa na matatizo makubwa ya magonjwa na hasa msongo wa mawazo.
Katika risala yao mabinti hao wameitaka serikali kufanyakazi yake kukabiliana na ubabe unaofanywa na viongozi wa kimila wa kuwalazimisha kukeketwa hata msimu unapokuwa umepita.
Mabinti hao ambao wengi wametoka shule ya msingi na sekondari wameweza kuwekwa hapo kwa msaada wa UNFPA ambao wametoa hela kupitia Children’s Dignity Fund (CDF), .Wafadhili wengine ni Daughters of Charity of St. Vincent Du Paul, na Askofu wa kanisa katoliki dayosisi ya Musoma, Michael Msongazila
DSC_0495
Mgeni rasmi Waziri wa Kazi na Ajira Mh. Gaudentia Kabaka akisalimiana na Mhashamu Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Musoma Mkoani Mara, Michael Msongazila mara baada ya kuwasili kwenye mahafali hayo.
DSC_0504
Kwaya ya vijana ya mara ikiimba wimbo wa Taifa kabla ya kuanza kwa sherehe za mahafali ya sita ya kituo cha kupambana na ukeketaji Masanga wilayani Tarime mkoani Mara.
DSC_0547
Mgeni rasmi Mh. Kabaka, Bw. Alvaro Rodriguez na SSP. Simon Mrashani wakishiriki kucheza wimbo maalum unaohamasisha kukataza vitendo vya uovu vya Ukeketaji kwa watoto wa kike wakati wa mahafali hayo.
DSC_0499
Meza kuu ikitoa heshima kwa wimbo wa taifa.
DSC_0555
Mkurugenzi wa Kituo cha kupambana na ukeketaji cha Masanga (TFGM), Tarime, mkoani Mara, Sista Germaine Baibika akimkaribisha mgeni rasmi pamoja wageni waalikwa kwenye sherehe ya mahafali ya sita ya mabinti waliokwepeshwa msimu wa ukeketaji.
DSC_0541
Mgeni rasmi Waziri wa Kazi na Ajira Mh. Gaudentia Kabaka akifurahi jambo na Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez kwenye sherehe za mahafali hayo.
DSC_0617
Mgeni rasmi Waziri wa Kazi na Ajira Mh. Gaudentia Kabaka akizungumza kwenye sherehe za mahafali ya sita ya mabinti waliokwepeshwa msimu wa ukeketaji.
DSC_0585
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akitoa salamu za Umoja wa Mataifa katika sherehe za mahafali sita ya mabinti waliokwepeshwa msimu wa ukeketaji.
DSC_0630
Mkuu wa Wilaya ya Tarime, mkoani Mara, Bw. John Henjewele akitoa salamu kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mara katika mahafali ya sita ya kituo cha kupambana na ukeketaji cha kijiji cha Masanga (TFGM) cha wilayani Tarime, mkoani Mara.
DSC_0557
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA), Dkt Natalia Kanem, akizungumza kwenye sherehe hizo.
DSC_0702
Kaimu kamanda wa polisi wa kanda maalum ya Tarime na Rorya SSP. Simon Mrashani akieleza jinsi jeshi la polisi linavyoshiriki katika kupambana na masuala ya unyanyasaji wa kijinsia likiwemo suala la kesi za ukeketaji ambapo pia alitoa takwimu za kesi zilizoripotiwa kituoni mpaka sasa ni 141, huku 80 zikiwa Mahakamani na 20 zimetolewa hukumu.
DSC_0552
Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu akifurahi jambo na baadhi ya wafanyakazi wenzake wakati wa sherehe za mahafali hayo.
DSC_0599
Wahitimu 37 wakila kiapo cha kutokubali kutoshiriki kukeketwa na kuwa mabalozi wazuri kwenye jamii zao katika kuelemisha madhara ya ukeketaji kwa wanaoendeleza mila na tamaduni hizo pindi warudipo majumbani. Kwa picha zaidi ingia humu

No comments: