ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, January 18, 2015

TASWIRA,MWIGULU NCHEMBA ATIKISA MKOA WA MOROGORO WOTE KWA SIKU MOJA

Mh:Mwigulu Nchemba akizungumza na Wananchi wa Gairo hii leo,Amesisitiza kuwatatulia swala la maji ambalo bajeti yake imeshaanza kufanyiwa kazi.Naibu katibu Mkuu akizungumza na wananchi wa Mvomero hii leo,Tatizo la Sukari ndio AGENDA kuu hapa Mvomero,Wananchi wanasumbuliwa na tatizo la soko la sukari na Migogoro ya Mashamba.Mwigulu Nchemba ameahidi kuchukua hatua kuhakikisha tatizo linapata dawa ya Kudumu.Mh:Mwigulu Nchemba akisalimiana na Mbunge wa Kilosa MH:MKulo hii leo mara baada ya kuwasili.
Mh:Mwigulu Nchemba akisalimiana na wananchi wa Mvomero.Mh:Mwigulu Nchemba akisalimiana na
wananchi wa kisaki hii leoWananchi wa Kimati wakifurahia ujio wa Naibu Katibu Mkuu Mh:Mwigulu Nchemba.Mwigulu Nchemba akiondoka Kimati.Naibu katibu Mkuu akiwasili Morogoro Mjini hii leo wakati akihitimisha Ziara yake aliyoifanya kwa Mkoa wote wa Morogoro.Mjumbe wa NEC wa Nachingwea akizungumza na Wananchi wa Morogoro Mjini.Hisia za Wanafunzi wa Elimu ya Juu Mkoani Morogoro kwa Mh:Mwigulu NchembaMwenyekiti wa Mkoa wa Geita Ndugu.Josephat Msukuma akizungumza na wananchi wa Morogoro Mjini wakati wa ziara ya Naibu Katibu Mkuu.Naibu Katibu Mkuu CCM Bara akiwasalimia wananchi wa Morogoro Mjini hii leo.Comrade Mwigulu Nchemba akizungumza na Wananchi wa Morogoro Mjini,Mwigulu amesisitiza wananchi kusimamia Vizuri Mali za Umma hasa kwa Viongozi waliopewa dhamana,Pia amesisitiza wananchi kujiandikisha kwenye Daftari la kupiga kura.Mkutano Ukiendelea Morogoro Mjini.
Mwigulu Nchemba amehitimisha ziara yake ya Kutembelea Mkoa wa Morogoro wote hii leo kwa Kufanya Mkutano Mkubwa Morogoro Mjini.
Katika ziara yake Mh:Mwigulu Nchemba ambaye ni Naibu katibu Mkuu CCM Bara amesisitiza Wananchi kujitokeza kujiandikisha kwenye daftari la wapiga Kura,Amesisitiza Viongozi waliochaguliwa serikali za Mitaa kutumia dhamana waliyopewa kwa Maslahi ya Watanzania wote,Pia amesisitiza kuwa hakuna nafasi ya Kulea wezi wa Mali ya Umma,CCM hainamkataba na wezi wa mali ya Umma.Mtu anayeiba Fedha za umma,Mtu anayeiba Madawa Hospitalini,Mtu anayetumia madaraka yake Ovyo ni Mtu asiyevumilika,hastahili kujiuzuru tu,Ni lazima hatua za Kimahakama zifuatwe na afilisiwe.
Mwisho,Mwigulu Nchemba amesisitiza kuwa CCM imetekeleza Ilani yake vizuri sana na bado wanaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya Maendeleo,hivyo Watanzania waendelee kuwa na Imani na chama cha Mapinduzi.

No comments: