Advertisements

Monday, January 5, 2015

WAISLAMU TANZANIA WAUNGANA NA WENZAO DUNIANI KUSHEREHEKEA MAULID YA MTUME MUHAMMAD (SAW)

Wanafunzi wa Madrasatul Dhuriyatul Islamia kutoka Kisiwani Tumbatu Mkoa wa Kaskazini Unguja wakisoma Qaswida wakati wa sherehe za Maulid Matukufu ya kuzaliwa bwana Mtume Muhammad (S.A.W.) zilizofanyika jana katika viwanja vya Maisra Suleiman Mjini Unguja mbele ya mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein,
Ustadh salum Rashid kutoka Amani Wilaya ya Mjini Unguja akisoma Mlango wa Barzanji(4) wakati wa sherehe za Maulid Matukufu ya kuzaliwa bwana Mtume Muhammad (S.A.W.) zilizofanyika jana katika viwanja vya Maisra Suleiman Mjini Unguja mbele ya mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi (katikati) Makamo wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif,Kadhi Mkuu wa zanzibar Sheikh Khamis Haji (kulia) Waziri wa katiba na Sheria Abubakar Khamis Bakary akifuataiwa na makamo wa Pili wa Rais Alhaj Seif Ali Iddi wakisimaa kwa pamoja na waislamu wengine na Viongozi wakati wa Kumswalia Bwana Mtume Muhammad S.A.W.katika sherehe ya Maulid iliyofanyika jana viwanja vya Maisra Suleiman Mjini Unguja
Baadhi ya waumini waliohudhuria maulid hiyo Picha kwa hisani ya K-VIS Blog.

1 comment:

Anonymous said...

mashallah hii ndo inavyotakiwa muwe kitu kimmoja waislamu na msiwe mfisadi kama wale wanginewe wadini inginewe.

mashallah maulid kareem.