Na Mwandishi wetu, Washington, DC
Kitendo cha Watanzania wa Massachusetts cha kujitokeza kwa wingi kwenye kisomo cha Rashid Mkakile ndicho kilichonipa msukumo na kuandika haya ya kwangu kutoka rohoni, sio kwa nia mbaya bali ni kujivunia Utanzania wangu na Wabongo wa Massachusetts wameninifundisha jambo ambalo siku zote kichwani mwangu nilifikiria halitawezekana kwenye Jumuiya zetu za Kitanzania zilizo mbali na nyumbani.Maisha niliyokulia mimi ni maisha ya kuwa karibu na ndugu, jamaa na rafiki wanao nizunguka kwa shida na raha hata kama ni ndugu,jamaa na rafiki wa kumsikia. Hili la ndugu, jamaa na rafiki wa kumsikia limekua changamoto kwa Jumuiya nyingi wa Watanzania waishio nje ya Bongo.
Nimeishahudhuria matukio mengi ya Massachusetts iwe misiba, visomo na matukio mbalimbali ya furaha, Watanzania wa huko wanatofauti kubwa na Watanzania wengine katika majimbo mengi hapa Marekani. Siku zote nilizohudhuria matukio yao, Watanzania walijitokeza kwa wingi lakini siku zote haikuniingia akilini kwamba hicho ninanchokiaona kwa Watanzania Massachusetts ni upendo zaidi kuliko mshikamano.
Ilikua ni siku ya Ijumaa Januari 16, 2015 usiku mimi, Mayor Mlima, Eliud Mbowe na Kessy Matairi kama anavyojulikana na wengi tukiwa pamoja na vijana wawili mtoto wa Kessy na mpwa wake tulianza safari ya kuelekea Massachusetts kwenda kumjulia hali Rashid Mkakile na kushiriki kwenye kisomo cha kumwombea apone haraka kilichofanyika siku ya Jumamosi Januari 17, 2015 kwenye mji wa Boston jimbo hilo la Massachusetts.
Tuliwasili salama asubuhi hio ya Jumamosi ya siku ya kisomo na baada ya mapumziko ya saa kadhaa, tulielekea kwenye hoteli aliyokua anaishi Rashid Mkakile kwa ajili ya kumjulia hali na pia kujua maswahibu ya ugonjwa wake yalivyoaanza.
Tulifika kwenye mji unaoitwa Revere kwenye hotel ya Rodeway Inn aliyokua akiishi ndugu yetu Mkakile baada ya kutoka Hospitali ya Beth Israel Deaconess Medical Center alipokua akipatiwa matibabu baada ya kupata Stroke wakati alipokuwa kikazi jimbo hilo lenye Watanzania wakarimu.
Tulipoingia chumba cha Mkakile alitupokea kwa uchangamfu sana huku akiwauliza jamaa na marafiki wa DMV wanavyoendelea. Kwa kuwarudisha nyuma ni kwamba Rashid Mkakile alishawahiishi DMV kwa miaka mingi ya nyuma na hivi sasa amehamia Dallas Texas na kilichompeleka Massachusetts ni kazi yake ya uendeshaji wa malori makubwa ya matairi 18.
Baada ya kujuliana hali tulitaka kujua kilichompata ndipo alipoaanza kwa kusema"ilikua ni mwezi Oktoba nilipokua Massachusetts wakati nikiwa nimeegesha lori nikiwa mimi na msaidizi wangu, nilisimama kutafuta kitu kwenye kabati ya lori juu na bahati mbaya nilijigonga kwenye hilo kabati ndani ya gari ndipo nilipoaanza kujisikia vibaya na kumwambia msaidizi wangu aite gari la wagonjwa ili nikachekiwe zaid hospitali".
Rashid aliendelea kwa kusema "baada ya kufika hospitali ndipo walipogundua kupasuka kwa mshipa mmoja wapo kwenye kichwa na kupelekea kunikimbiza kwenye chumba cha upasuaji kuokoa maisha yangu". Baada ya kufanyiwa upasuaji na kuendelea kukaa hospitalini, Rashid Mkakile aligunduliwa na dada wa Kitanzania anayefanyakazi kwenye hospitali hiyo baada ya kusoma majina ya wagonjwa na kuona jina la Mtanzania ndpo alipomjulisha kiongozi mmoja wa Jumuiya ya Watanzania Massachusetts ajulikanae kwa jina la Salum.
Baada ya Salum kupata taarifa za Mtanzania mwenzao kulazwa jimboni mwake na mbali na kutoa taarifa kwenye kwa Watanzania wengine waishio Massachusetts, alikua akienda kumjulia hali Rashid Mkakile kila siku,
Watanzania wa Massachusetts nao baada ya taarifa za mgonjwa kuwafikia kwa wingi na walijazana kwenye chumba cha mgonjwa kila siku huku wakiendelea kuwasaidia ndugu, jamaa na marafiki wa Mkakile waliokuwa wakienda Massachusetts kumwangalia ndugu yao.
Walichokifanya Watanzania hawa ni cha kuigwa na Watanzania wote, Huku tulipo ni mbali ni Utanzania wetu pekee na kuongea lugha moja ndio silaha yetu kubwa ya Upendo na Mshikamano.
Siku ya kisomo ndipo pia kulikonishangaza kuona Watanzania wa Massachusetts kujitokeza kwa wingi pamoja na kwamba kulitokea kwa wenye ukumbi kuchelewa kufungua ukumbi kwa saa tatu lakini pamoja na baridi kuwepo Watanzania wa Massachusetts walisubili mpaka saa zote hizo kuanzia saa 10 jioni mpaka saa 1 usiku ukumbi ulipofunguliwa na kumfanyia kisomo Rashid Mkakile Mtanzania wasie mjua walichounganishwa nae ni upendo na kujali Utanzania wa kuongea lugha moja.
Upendo huu wa Watanzania Massachusetts umenifanya kujiuliza maswali mengi yaliyokua na jibu moja la kwamba matatizo yanapokufika hayachagui ndugu, jamaa wala rafiki na sisi tuliombali na nyumbani tutambue ndugu yangu, jamaa yangu na rafiki yangu ni wewe tunaeishi na maisha yetu ya kila siku ya kupiga box.
Nahii ndio sababu ya kusema ninatamani na mimi ningekuwa Mtanzania niayeishi Massachusetts nawaombea kwa Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema awajalie yote yaliyomema na awazidishie upendo na mshikamano zaidi ya hapo na mwendelee kuwa kitu kimoja kama Watanzania.
No comments:
Post a Comment