ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, February 11, 2015

Mauaji ya wanafunzi waislamu yazua hisia


Maafisa wa polisi mjini Carolina kazkazini nchini Marekani wamemkamata mtu mmoja baada ya wanafunzi watatu waislamu kupatikana wamefariki nyumbani mwao.
Miili ya Deah Barakat,mkewe Yusor Mohammed Abu salha na dadaake Razan Mohammed Abu salha ilipatikana siku ya jumanne ikiwa na majeraha ya risasi katika vichwa .

Mtu mmoja mwenye umri wa miaka 46 tayari amefunguliwa mashtaka kutokana na mauaji hayo.

Maafisa wa polisi wanasema wanajaribu kubaini iwapo mauaji hayo yanatokana na chuki.

Swala kwamba wanafunzi waliouawa ni waislamu limezua uvumi katika mitandao ya kijamii wa iwapo mauaji hayo ni ya kidini au la

Uchunguzi uliofanywa umebaini kwamba uhalifu huo ulitekelezwa kutokana na mzozo unaondelea kuhusu uegeshaji wa magari,maafisa wa polisi wa Chapell wamesema.

1 comment:

Anonymous said...

mmhuuu, kisa mzozo wa kuegesha magari, na kama hawa wanafunzi wangekuwa ndio walouwa basi story ingekuwa ni brutal terrorists. sawa sisi tunaangalia tu maana kule ufaransa charlie alipokuwa akimtukana na kumdhihaki mtume Muhammad walisema freedom of speech, na juzi katokea mtu kumdhihaki huyo charlie basi amekamatwa na sasa anashtakiwa kwa blasphemy!!dunia hiii