Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akitoa hotuba katika mkutano wa kujadili namna ya kujiandaa kukabiliana na maafa mbalimbali yanayoweza kutokea Mkutano uliofanyika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mbweni Zanzibar.
Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mohammed Aboud Mohammed kitoa hotuba yake katika mkutano wa kujadili namna ya kujiandaa kukabiliana na maafa mbalimbali yanayoweza kutokea Mkutano uliofanyika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mbweni Zanzibar
Baadhi ya Viongozi wa Nchi Tano za mataifa mbalimbali walioshiriki katika mkutano wa kujadili namna ya kujiandaa kukabiliana na maafa mbalimbali yanayoweza kutokea Mkutano uliofanyika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mbweni Zanzibar.
Kamanda Philip Knightsheen akitoa salamu za Shirika lake linalosimamia huduma za Kibinaadamu na Afya la Usafricom kwenye mafunzo ya siku tano ya zoaezi la kukabiliana na maafa Zanzibar hapo Zanzibar Beach Resort Mazizini.
Mwakilishi wa shirika la Misaada la Marekani Us Aid Bibi Anna Senga akizungumza katika mafunzo ya siku tano kuhusu zoezi la kukabiliana na maafa Zanzibar.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Moh’d Aboud Moh’d akimkabidhi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Ripoti ya Maafa Zanzibar.
Mkurugenzi wa Idara ya Maafa Zanzibar Nd. Ali Juma Hamad wa kwanza kutoka kulia akiwa na baadhi ya watendaji wa Idara hiyo wanaoshiriki mafunzo ya sku tano kuhusu zoezi la kukabiliana na maafa Zanzibar.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya siku tano kuhusu zoezi la kukabiliana maafa Zanzibar yanayofanyika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini.
Mwakilishi wa shirika la Misaada la Marekani Us Aid Bibi Anna Senga akibadilishana mawazo na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif nje ya ukumbi wa Zanzibar Beach Resort mara baada ya kufunguliwa rasmi mafunzo ya zoezi hilo.
Balozi Seif ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais ,Tawala za Mikoa na Idara Maalum Mh. Haji Omara Kheir. Kulia ya Balozi Seif ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Moh’d Aboud Moh’d na Mwakilishi waShirika linalosimamia huduma za Kibinaadamu na Afya la Usafricom Kamanda Philip Knightsheen.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo ya siku tano kuhusu zoezi la kukabiliana na maafa Zanzibar yanayofanyika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort. kushoto ya Balozi Seif ni Mwakilishi wa shirika la Usafricom Kamanda Philip Knightsheen, Waziri wa Afya Zanzibar Mh. Rashid Seif , Kaimu Kamanda wa Brigedia Nyuki Zanzibar na Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mh. Abdulla Mwinyi. Picha na OMPRZ











No comments:
Post a Comment