
Bobbi Kristina alikutwa ameanguka bafuni huku kichwa kikiwa kikiwa ikimeinamia chini na kuonekana na michubuko kitu ambacho kimepelekea polisi kufanya uchunguzi wao kwa kumhoji mchumba wake Nick Gordon na rafiki yao aliyekuwepo siku ya tukio. Nick Gordon ni mtoto aliyelelewa na Whitney Houston tangia alipokua na miaka 9 na kuingia na mahusiano ya mapenzi na Bobbi Kristina ambaye ni mtotoi wa Whitney Hoston aliyezaa na Bobby Brown. Marafiki wa wawili hao wamedai wapenzi hawa wameishakua na maugomvi huko nyuma kitu wanachodai ni kutokana na wivu alionao Nick Gordon kwa Bobbi Kristina.
Shangazi wa Bobbi Kristina aliomba Dunia waendelee kumwombea Bobbi Kristina aendelee kupata nafuu na kupona kabisa kwani imekuwa ni wakati mgumu kwa familia na maumivu hasa kwa baba yake Bobby Brown. Bobbi Kristina bado yupo kwenye mashine katika hospitali ya chuo kikuu cha Emory jimbo la Georgia.
No comments:
Post a Comment