Meneja Mradi wa Kamati ya Uangalizi wa Chaguzi Tanzania (TEMCO), Dk Benson Bana
Meneja Mradi wa Kamati ya Uangalizi wa Chaguzi Tanzania (TEMCO), Dk Benson Bana, amesema kuwa fedha hizo zilizotolewa na USAID lengo lake hasa ni kuwawezesha waangalizi kutambua uozo pamoja na mambo mema yaliyofanyika kwenye michakato hiyo na kujua kama yalifanyika kwa haki.
Shirika la Misaada la Marekani (USAID) limetoa fedha kiasi cha Sh720bilioni maalumu kwa ajili ya kuwawezesha waangalizi wakati wa mchakato wa uandikishaji wapiga kuwa, kura ya maoni na Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Octoba mwaka huu.
Meneja Mradi wa Kamati ya Uangalizi wa Chaguzi Tanzania (TEMCO), Dk Benson Bana, amesema kuwa fedha hizo zilizotolewa na USAID lengo lake hasa ni kuwawezesha waangalizi kutambua uozo pamoja na mambo mema yaliyofanyika kwenye michakato hiyo na kujua kama yalifanyika kwa haki.
Amesema kwa mara ya kwanza kamati hiyo, pia itaangalia mchakato wa uteuzi wa wagombea ndani ya vyama vya siasa, utakaojumuisha wagombea urais, ubunge, ujumbe wa Baraza la wawakilishi na udiwani.
Baada ya kumalizika kwa zoezi hilo, TEMCO itaandika ripoti itakayoweka wazi mbinu mbalimbali zinazotumiwa na wanasiasa kuteua na kushinda nafasi wanazogombea ikiwamo kununua kura.
“Watazamaji wa uchaguzi watakuwa makini kuangalia mifumo ya kisheria na kitaasisi, uteuzi wa wagombea ndani ya vyama vya siasa, uthabiti wa tume za uchaguzi, utekelezaji wa Sheria ya gharama za Uchaguzi na uteuzi wa wagombea unafanywa na tume za uchaguzi,” amesema Dk Bana.
Dk Bana amesema zoezi hilo lililofadhiliwa na Shirika la Misaada la Marekani (USAID), litasimamiwa na watazamaji wa muda mrefu 180 watakao angalia zoezi la uandikishaji wapiga kura litakaloanza Februari mwaka huu.
Watazamaji wa muda mfupi 6,400 wanatarajiwa kuangalia shughuli za kila siku ya kupiga kura ya maoni, Uchaguzi Mkuu utaangaliwa na watazamaji wa muda mrefu 118 na 7,000 wa muda mfupi watakaopangwa katika vituo mbalimbali Tanzania Bara na Zanzibar.
No comments:
Post a Comment