Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Balozi Seif Ali Iddi akiwa sambamba na Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Taifa Mzee Ali Hassan Mwinyi wakikata utepe kuashiria kuzinduliwa kwa Jengo la Ofisi ya Tawi la CCM la Kijiji cha Ghana Jimboni Uzini Mkoa wa Kusini Unguja.
Balozi Seif akiwa na Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Kusini Unguja aliyepo Kati kati Dr. Idriss Muslim Hijja na Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Mh. Moh’d Raza wakifurahia mazingira safi ya Ofisi Mpya ya CCM Tawi la Ghana mara baada ya kuzinduliwa rasmi.
Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Mh. Moh’d Raza akielezea umuhimu wa wana CCM kuendelea kushirikiana pamoja ili kupata faraja wakati wa hafla fupi ya kuzinduliwa kwa Ofisi ya Tawi la CCM Ghana Mkoa wa Kusini Unguja.
Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Taifa Mzee Ali Hassan Mwinyi akiwanasihi Wananchi kuendelea kuheshimu Historia ya Kijiji cha Ghana kiliopo Wilaya ya Kati ambacho kilihusika kikamilifu katika maandalizi ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Mwaka 1964.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Wana CCM na Wananchi wa Kijiji cha Ghana ndani ya Jimbo la Uzini mara baada ya kulizindua Tawi lao jipya.
Kulia ya Balozi Seif ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja Nd. Ramadhan Abdullah Ali, kushoto ya Balozi Seif ni Mwenyekiti wa CCM Tawi la Ghana Ndugu Daud Haji Hassan pamoja na Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Kusini Unguja Dr. Idriss Muslim Hijja.
Mandhari nzuri ya kupendeza inayoonekana ya Jengo la Ofisi ya CCM Tawi la Ghana liliopo Jimbo la Uzini, Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja.
Picha na – OMPR – ZNZ.






No comments:
Post a Comment