Lori lililosababisha ajali na kuua mwanafunzi na kusababisha wanafunzi wa shule za msingi Tunduma kulala barabarani wakishinikiza kuwekwa kwa matuta.
Baadhi ya wanafunzi wa shule za Msingi Umoja,Mlimani na Tunduma za mjini Tunduma wakiandamana kushinikiza kuwekwa matuta kwenye inayoelekea Sumbawanga kutokana na ajali za mara kwa mara zinazosababishwa na mwendo kasi wa madereva.
Lori linaloonekana pembeni limepinduka, limesababisha ajali na kuua mwanafunzi.
Lori linaloonekana pembeni limepinduka, limesababisha ajali na kuua mwanafunzi.
Askari wa usalama Barabarani mjini Tunduma akipewa maelezo ya hali ya mtoto aliyejeruhiwa katika ajali hiyo Jackson Sichalwe(7) kutoka kwa baba yake Mzazi Norbert Siichalwe,Mtoto Jackson amelazwa katika hospitali ya serikali mjini Tunduma baada ya kugongwa na gari ambalo pia lilisababisha kifo cha Emmanuel Sichalwe mwanafunzi wa shule ya msingi Umoja ya mjini Tunduma
Mamia ya wakazi wa mji mdogo wa Tunduma wakiwa katika mkusanyiko kufuatia taharukii iliyoibuka mjini i
Diwani wa Kata ya Tunduma Frank Mwakajoka akizungumza na wanaanchi baada ya kutokea tafrani iliyosababisha wanafunzi wafunge barabara kwa kushinikiza kuwekwa matuta.Picha na Rashid Mkwinda
SAUTI zilizochanganyika na hisia na majonzi kutoka kwa wanafunzi wa shule tatu za Msingi, Umoja, Mlimani na Tunduma zilisikika hewani na kutoa ujumbe ulioashiria kupata ufumbuzi wa tatizo la ajali za mara kwa mara katika barabara kuu iendayo Sumbawanga kutokea mjini Tunduma.
Ijapokuwa zilikuwa ni sauti za watoto, zilibeba ujumbe mzito wenye shinikizo la uchungu uliofuatia kufariki kwa mtoto mwenzao Emmanuel Sichalwe (7) ambaye aligongwa na lori na kufariki hapo hapo baada ya kukanyagwa na kupasuka kichwa.
Haikuwa rahisi kuhisi machungu ya watoto hao ambao ni kilio cha muda mrefu kutoka kwa wazazi na wananchi waishio maeneo ya barabara kuu ya kuelekea Sumbawanga ambapo takribani watu 18 wakiwemo watoto 10 na watu wazima 8 hali ambayo imekuwa ikijenga hofu miongoni mwa wakazi wa maeneo hayo.
Wanafunzi hao walifunga barabara na kulala barabarani kuanzia saa 12:30 alfajiri huku wakihanikiza sauti zao hewani kwa maneno yaliyosikika, "Tunataka!!, Matuta!!. Magari!!, Yanatumaliza!!!" sauti hizo zilikaririwa mara kwa mara huku baadhi yao wakionesha mabango.
3 comments:
This is activism at an ealry age for a good coause. Matuta pleaseee
hakuna cha matuta wala nini mi vibwaga vya kichawi hivi wanataka kunywa damu za watu kwa wingi so wanatengeneza maajali kama haya nchi hii wakuu wa nchii hii wanatumia sana utaalamu wa giza.so hata wakiweka matuta,kuziiti mwendo luku,kupimwa kama umelewa kwa kitaalamu hakuna kitu hapo.
hii kitu mbaya sana wanachofanya hawa watu wabaye washindwe na kuregaa kwa damu ya yesu amen.
hakuna cha matuta wala nini mi vibwaga vya kichawi hivi wanataka kunywa damu za watu kwa wingi so wanatengeneza maajali kama haya nchi hii wakuu wa nchii hii wanatumia sana utaalamu wa giza.so hata wakiweka matuta,kuziiti mwendo luku,kupimwa kama umelewa kwa kitaalamu hakuna kitu hapo.
hii kitu mbaya sana wanachofanya hawa watu wabaye washindwe na kuregaa kwa damu ya yesu amen.
Post a Comment