ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, February 21, 2015

WAZIRI CHIKAWE NA MWANA FA WATEMBELEA UBALOZI WETU MAREKANI

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kulia) akizungumza na mwanamuziki mkongwe wa Bongo Flava, Hamis Mwinjuma maarufu kama Mwana FA wakati mwanamuziki huyo alipokutana na Waziri huyo jijini Washington DC katika Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani. Waziri Chikawe yupo nchini humo kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Kimataifa wa Kupambana na Vurugu na Ugaidi duniani, na kwa upande wa Mwana FA yupo nchini Marekani kwa ajili ya matembezi yake binafsi hata hivyo alienda ubalozini hapo kwa ajili ya kumsalimia Balozi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (wapili kulia), Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Liberata Mulamula wakiwa katika picha ya pamoja na mwanamuziki mkongwe wa Bongo Flava, Hamis Mwinjuma maarufu kama Mwana FA wakati mwanamuziki huyo alipokutana na Waziri huyo jijini Washington DC katika Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani. Waziri Chikawe yupo nchini humo kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Kimataifa wa Kupambana na Vurugu na Ugaidi duniani, na kwa upande wa Mwana FA yupo nchini Marekani kwa ajili ya matembezi yake binafsi hata hivyo alienda ubalozini hapo kwa ajili ya kumsalimia Balozi. Kulia ni rafiki wa mwanamuziki huyo ambaye pia ni mfanyabiashara, Salah Saidi. Picha zote na FelixMwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

1 comment:

Anonymous said...

mmependeza kwenye hii picha .Yetu macho.waka huu kunapokaribia uchaguzi tutayaona mengi na kuyasikia mengi.sarakasi zimeshaanza kwa sana huko marekani marekani.wenye akili zao na ufahamu wa hali ya juu wanajua kinachoendelea huko na wanachotaka kukifaya huko kwa wana diaspraa. mujini mujini shule.