Gavana wa BoT, Profesa Benno Ndulu.
Wizi wa fedha kwa njia ya mtandao kupitia mashine maalum za kutolea fedha (ATM) unaendelea kuzitesa benki mbalimbali nchini ambapo kwa sasa wahalifu hao wanahamisha fedha za wateja wakiwa nje ya nchi kwa kutumia kadi za kutolea fedha.
Wizi huo hufanyika kwa kutumia kadi za kutolea fedha zinazoingiliana na benki zingine (smart card) ambazo mteja wa benki anaweza kutolea fedha akiwa popote duniani kupitia ATM.
Chanzo chetu cha habari kimetufahamisha kuwa wezi hao hucheza za nywira (password) za watu wanaopenda kutoa fedha zao kupitia ATM zilizowekwa sehemu mbalimbali hasa kwenye vituo vya kujazia mafuta (petrol stations)
Chanzo chetu cha habari kilichokumbwa na mkasa wa kuibiwa fedha (jina linahifadhiwa) kiliiambia NIPASHE kuwa, juzi alipigiwa simu na ofisa mmoja wa benki akiumuuliza kama siku hiyo alikuwa ametoa fedha akiwa nje ya nchi.
Alisema ofisa huyo alimpigia simu baada ya benki kupata wasiwasi kwa kuwa taarifa hazionyeshi kama mteja huyo huchukua kiasi hicho kikubwa cha fedha kwa mara moja.
“Nlinipigiwa simu na mtu akaniuliza wewe ni fulani (akitaja jina), akaniuliza nimetoa fedha kiasi fulani nikiwa Mombasa? Nikamjibu sijatoa na sijawahi kutoa fedha nje,” alisema.
Chanzo hicho kilisema, ofisa huyo alimwambia kuna hamisho la fedha limefanyika kutoka kwenye akaunti yake nje ya nchi na hivyo kumtaka aende kwenye tawi lolote la benki hiyo ili aombe taarifa yake ya kibenki na kisha aandike barua ya kulalamika kuwa hajatoa fedha hizo kwenye akaunti yake.
Alisema kwa kuwa alikuwa maeneo ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, aliamua kwenda kwenye tawi lililopo eneo hilo na huko aliomba apewe taarifa yake ya kibenki ya mwezi mmoja.
“Nilipoitazama nikaona fedha zangu zimehamishwa na mtu aliyekuwa Mombasa, Kenya,” alisema na kuongeza kuwa alitakiwa kuandika barua kwa meneja wa benki hiyo wa tawi hilo, ambapo alitakiwa ataje akaunti yake, kiwango cha fedha kilichotolewa na eleze kuwa fedha hizo hakuzitoa yeye na aombe kurejeshewa.
Alisema wakati huo akaunti yake ilikuwa imefungwa na kadi imezuiwa kutoa fedha na kutaka kujaza fomu ya kupata kadi nyingine ambayo alipewa ndani ya dakika tano.
Aliongeza kuwa baada ya kukamilisha taritibu za madai ilipata taarifa iliyomjulisha kuwa fedha zake zitarudishwa ndani ya siku 45.
NIPASHE ilipotaka kufahamu kuhusu wizi huo, ilizungumza na afisa mmoja wa benki ambaye hata hivyo, hakupenda jina lake litajwe gazetini na kukiri kuwa kuna wizi wa fedha wa mara kwa mara kwa njia ya mtandao ambao benki umeshaugundua.
Alisema wezi hao hutumia njia mbali mbali kujua password za watu ikiwemo ya kuweka kamera ndogo kwenye ATM na vile vile kwa kutumia utalaam wa kiteknolojia wa hali ya juu kusoma taarifa za benki na kuzitumia kuiba fedha kwenye akaunti za watu.
Alishauri wanaopenda kutoa fedha kwenye ATM waende kwenye ATM zilizo kwenye matawi ya benki husika kwa kuwa wanaoweka kamera sio rahisi kwenda kwenye matawi ya benki.
Aidha, aliwataka wateja kuwa na utaratibu wa kuangalia akaunti zao mara kwa mara ili kubaini kama kuna tofauti yoyote kwenye fedha zao.
NIPASHE ilipotaka kauli ya Waziri wa Fedha kuhusu wizi huo, simu yake haikuwa na majibu.
Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ilishawahi kukaririwa kuwa itaendelea kufanya utafiti wa kuwabana wezi hao.
Kauli hiyo ilitolewa na Gavana wa benki hiyo, Profesa Benno Ndulu, wakati akizungumzia wizi wa mitandao na kuongeza kuwa licha wa wizi huo kufanyika, huduma za kibenki zitaendelea kutolewa kwa kuwa ni mkombozi wa wateja.
Aidha, alisema wameziagiza benki kuweka kifaa cha umeme (electronic chip) kwenye kadi zao za ATM ambazo si rahisi kughushi.
Kauli hiyo ilifuatia baadhi ya wateja kutishia kufunga akaunti zao kuhofia wizi wa fedha zao.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment