Advertisements

Monday, February 2, 2015

Zari Hassan kufunga ndoa na Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, "Asema hakuna umri maalumu wa Kuoa au Kuolewa"!

WAKATI mama mzazi wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Sanura Kasim ‘Sandra’ akiwa nchini India kwa matibabu ya tatizo la kiafya linalodaiwa kuwa ni kupooza, hapa Bongo dalili za Diamond na mpenzi wake wa sasa, Zarinah Hassan ‘Zari’ au The Boss Lady kufunga ndoa zinanukia. 
Chanzo makini kimeliambia Ijumaa Wikienda kwamba, licha ya mama Diamond kupelekwa India Januari 27, mwaka huu na msafara wa watu wawili, nyuma, Zari alitua Bongo tangu Januari 30, mwaka huu lengo kubwa likiwa kumuuguza mama mkwe wake huyo.

ATUA DAR, AENDA SINZA-MORIChanzo kikazidi kuweka wazi kuwa mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Diamond alimpokea na kwenda naye nyumbani kwake, Sinza-Mori jijini Dar bila kumwambia kama mama yake amepelekwa India kwa matibabu.
“Diamond alikwenda kumpokea Zari lakini hakumwambia kama mama yake amekimbizwa India kwa matibabu na yeye (Zari) alikuja kwa lengo la kumuuguza mama mkwe wake,” kilisema chanzo.

BAADA YA KUMKOSA MAMA MKWEHabari zaidi zilisema kuwa, walipofika nyumbani na Zari kuambiwa mama Diamond amepelekwa India, aliumia sana na kumlaumu mpenzi wake huyo kwa nini hakumwambia kuhusu safari ya mama tangu walipokutana uwanja wa ndege.

YAISHA, DIAMOND AMPELEKA ZARI KWENYE UJENZIBaada ya kuwekana sawa kuhusu usiri wa safari ya mama’ke, Diamond alimchukua Zari na kumpeleka kwenye nyumba yake anayoijenga Mbezi-Beach, Dar kwa lengo la kumuonesha sehemu ya mali zake ambapo ilisemekana nyota huyo wa Uganda aliipenda ramani ya nyumba hiyo.

ZARI AGOMA TENA KULALA HOTELINIKatika siku za hivi karibuni, tuliwahi kuandika kuwa Zari alilala kwa mama Diamond, akapika na kupakua ambapo mawifi zake walimsifia.
Hata katika ujio wake wa Juni 30, mwaka huu, mrembo huyo mwenye utajiri mkubwa aligoma kwenda kulala hotelini na kumwambia Diamond atalala naye nyumbani kwao, Sinza-Mori.

ZARI AANZA KUBADILI DINI?Zari ni Mkristo wa Kanisa la Born Again ambalo ni la kiroho nchini Uganda. Aliingia kwenye imani hiyo baada kuokoka na kubatizwa kwa maji mengi kama Biblia inavyotaka lakini kwa kuwa na Diamond kuna dalili za kuanza kubadili imani ili kutimiza mipango ya ndoa.
“Ukiachia kwenda kwenye nyumba hiyo ya Mbezi pia Diamond ameshaanza kumfundisha Zari baadhi ya mambo ya kidini,” kilisema chanzo.

Ijumaa iliyopita ambayo kiimani, Diamond hupenda kuvaa mavazi ya Kiarabu ambayo hutafsirika ni ya Kiislam, Zari naye alitupia vazi la baibui ili kwenda sawasawa na mwandani wake huyo.

WAENDA SONGEA WOTEWakati Ijumaa Wikienda likijiandaa kwenda mitamboni, habari za moto ni safari ya Diamond kwenda mjini Songea ambapo ni makao makuu ya Mkoa wa Ruvuma.
Diamond alikwenda kwa ajili ya shoo ya sherehe za Chama cha Mapinduzi (CCM) kutimiza miaka 38 tangu kuasisiwa kwake. Sherehe hizo zilifanyika kwenye Uwanja wa Majimaji jana.

ZARI KWAPANIHabari za uhakika ni kwamba, katika safari hiyo, Diamond alimuweka Zari kwapani na kwenda naye kwa lengo la kumpa kampani.

DIAMOND: KILA KITU KINA WAKATI WAKEIjumaa Wikienda lilimtafuta Diamond kwa njia ya simu ambapo awali alikiri mama yake kupelekwa India kwa matibabu. Kuhusu Zari kubadili dini, kuvaa hijabu na kufunga ndoa, alisema: “Mbona mna maswali sana jamani, kila kitu kina wakati wake.”

15 comments:

Anonymous said...

Do go hawezi kumudu lifestyle ya huyu dada for long with a peanut money he has. It's just the matter of time.

Anonymous said...

wanawake wazuri wazuri wameolewa yamebaki makurumbembe yanahangaika naimba tu lakini huu wimbo una ukweri ndani yake tunayaona hapa dc

Anonymous said...

Makurumbebe wapi labda uliye naye ndo kurumbembe huna ubavu wa ku deal na hao wasio olewa na ki ukweli wanawake wazuri ndo wahajaolewa.

Makurumbebe ndo walio olewa mpaka mume anatoka nje kuwa na nyumba ndogo na cha kuchekesha huwa anamzalisha huyo wa nyumba ndogo huku anaye huyo mke Kurumbembe boya.

wanawake wazuri ndo wako single na wanangara kila leo mwanamke alieolewa hata mvuto hana.

mcheki zari kaa separate na anakula raha na Serengeti boy wake.Alivyokuwa ndani ya ndoa balaa tupu na kunyimwa uhuru wake.

single lady kila mwanamme anamtamani na anatamani angekua wake ili aje amfisidi kwakumuweka ndani na kumzalisha ovyoo na kumfanya mashine yakutaga mayai.

kila leo akitoka nje anakutana na ma baby wa high class anaishia KUWAKODOLEA MIMACHO NA TAMAA YA FISI na kumuona wake wa ndani KURUMBEMBE NA NDO MWANZO WA MCHEPUKO UNAPOANZA.

GET REALLY DUDE SINGLE LADIES WANAJIPENDA NA WANAPENDEZA NA KUPENDWA. KILA WANAPOPAPITA MITAANI HAWANUKI MAZIWA YA KUNYONYESHA VICHANGA KILA LEO.

UMEZIKOSA HIZO NDIZI WEWE SUNGURA MJANJA UNASINGIZIA SIZITAKI MBICHI NA HUYU DEMU KURUMBEMBE;KUMBE WAPI UNGEZIPATA UNGEFURAHIYA.

SINGLE LADIES KEEP IT UP MNAPENDWA KILA PEMBE YA HII DUNIA NA WALA NYINYI SI KURUBEMBE.

Anonymous said...

Wewe anoy wa 9.08 kimekutouch naona ungekuwa high class usingekua kurumbembe la pembeni aliempenda na kumuheshimu kamuoa wewe kurumbembe wanakuchezea tu. Na zari kwa taarifa yako sio kurumbembe mwenzako anaoelewa halooooo naomba tena wanawake wazuri wazuri wameolewa yamebaki makurumbembe yanahangaika yanahangaika yanahangaika

Anonymous said...

Hahaha wewe wa 6.44 pm kula tano eti makurumbembe mbona umelipandisha hasirA moja ndio huoni hata Aibu kujisifu kua side chick? Mume dawa babu wee

Anonymous said...

Hehehehehe ! DC na makurumbembe ! Jamani dada chepuke linajipa hope ! Mweee ! Jamani mnanichekesha! Hahahahaa ! Nishajipatia neno ! Side chick kurumbembe unalo hilo !

Anonymous said...

VITUKO MAKURUMBEMBE AISEE COMENTI MOJA TU UNACHANGANYIKIWA HIVYO? POLE DADA SIDE CHICK NI KIPOOZEO TU ANGEKUESHIMU ANGETANGAZA NDOA PUNGUZA HASILA NA WANANDOA !MMH

Anonymous said...

hehehehehe KUBWA LA MAKURUMBEMBE linatetea MAKURUMBEMBE wenzie.MIDA ISHAYOYOMA HIYO,MAKURUMBEMBEZZZZZ!!Hehehehee

MUKE YA MUTU.

Anonymous said...

Hahahahahaaaaa, You guys make my day..Eti side chick kurumbembe. Ila kuolewa raha lkn umpate anayejitambua.

Anonymous said...

kuolewa raha babu eeeeeeee halooooo utabaki na ukurumbembe wako hahhahhahhahahhahha. unalo.

Anonymous said...

hahahahaha warereeeeee mbona unalo we kubwa la makurumbembe. ungekuwa wa maana usingetumiwa guest house....hujishangai kupangiwa muda wa kupiga na kutuma massage....ujue yuko na muke/mwanamuke muzuri ndani. mxiuuuuuuuu.

Unknown said...

Saf

Unknown said...

Saf

Unknown said...

Saf

Unknown said...

Safiiiiiiiiiiii