ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, February 10, 2015

Zimamoto wajitetea ajali ya moto Dar

Dar es salaam, Siku tatu baada ya ajali ya moto kutokea  katika eneo la Kipunguni A jijini Dar es Salaam na kusababisha vifo vya watu sita na nyumba kuteketeatu, Jeshi la Zimamoto limejitete kuwa lilishindwa kufika haraka kwenye tukio kwa sababu ya ubovu wa mawasiliano kati yao na wananchi.
Katika tukio hilo, Emmanuel Mpira ambaye ni mtoto katika familia hiyo ndiye aliyenusurika kwani alikuwa matembezini ambapo aliporudi alikuta moto umeshaanza kuwaka na baadhi ya vitu vilishaanza kuteketea.
Inspekta wa Jeshi la Zimamoto, Puyo Nzalayaimis ameeleza kuwa wananchi wasiwalaumu kwa sababu taarifa zilichelewa kufika ofisini kwao na kuongeza kuwa mawasiliano yalikuwa mabovu.
Amesema alipokuwa anatoka kuelekea eneo la tukio walipotea njia na kuelekea hadi Kituo cha Polisi cha Sitaki Shari na badae wasamaria wema waliwaelekeza hadi eneo la tukio.
“Katika nyumba hiyo hakikuwezwa kuokolewa hata kitu kimoja kwasababu vitu vyote vilishaanza kushika moto na zima moto walipofika eneo la tukio waliweza kumalizia kuuzima na kutoa miili ya marehemu na kukabidhi kwa Jeshi la Polisi,”amesema Nzalayaimisi
Ameongezea kwa sasa jeshi hilo linakabiliwa na changamoto nyingi  ikiwemo uhaba wa  magari  , mawasiliano mabovu na kutojua mitaa mingi ya jijini Dar es Salaam.
Aliwashauri wananchi kutoa taarifa kamili na watu wanapojenga nyumba wahakikishe wanakuwa na milango na madirisha  ya dharula.
MWANANCHI

1 comment:

Anonymous said...

Itakuwa si haki kutupia lawama kikosi cha zimamoto kufuatia ajali hii.Serikali inapaswa kuboresha huduma hii muhimu kwa;
1.Kufuatia kuongezeka kwa idadi ya watu na makazi katika jiji la Dar,serikali inapaswa kufungua vituo zaidi vya zimamoto, at least 2 kila wilaya hapa Dar.
2.Mamlaka za kila wilaya,miji na majiji kwa kushirikiana na wizara ya ardhi wanapaswa kusimamia mpango bora wa mpangilio wa makazi.ambao utaweza kutoa access kwa huduma kama fire,ambulance etc ziweze kuwafikia wananchi kwa haraka.
3.Kuwekwe utaratibu kwa kuwa na proper address na zip codes aambazo zitawezesha ku-identify sehemu inayohitaji huduma kwa urahisi.
Kwa taarifa tu katika nchi zilizoendelea kituo kimoja cha fire kinahudumia watu kati ya 5,000 to 20,000 na response time ni kati ya dakika 4 mpaka 10.Sasa kwa ratio hii, Dar kituo kimoja kwa watu milioni 4 with poor logistics,sidhani ni haki kuwalwumu hawa jamaa.