Friday, March 13, 2015

BASI LA ARUSHA EXPRESS LAPATA AJALI ARUSHA

Basi la Arusha Express baada ya kupata ajali.
Taswira kutoka eneo hilo la ajali.

BASI la Arusha Express limepata ajali leo maeneo ya Uwanja wa Ndege wa Kisongo jijini Arusha wakati likijaribu kulipita gari ligine na kukutana na lori mbele yake.

Ili kuepesha madhara, dereva wa lori aliamua kuingia kichakani ili asigongane uso kwa uso na basi hilo.
Wananchi wakishuhudia ajali hiyo.


Katika ajali hiyo, hakuna aliyepoteza maisha isipokuwa watu ndani ya lori ndiyo wamejeruhiwa na kukimbizwa hospitali.

(Picha / Habari: Global Whatsapp 0753 715 779, kama una tukio tafadhali tutumie kupitia namba hiyo)

No comments: