Advertisements

Friday, March 6, 2015

DARAJA LA EDMUND PETTUS ALILOTUMIA DR KING KWA MATEMBEZI YA KUPINGA WEUSI KUTOKUPIGA KURA

Hili ndio daraja lililopo mji wa Selma jimbo la Alabama yalikofanyika matembezi yaliyoongozwa na Dr Martin Luther King mwaka 1965 kupinga Wamarekani weusi kutokupiga kura katika matembezi hayo ambayo mara ya kwanza yalishindwa baada ya polisi kuapiga Wamerekani weusi na wengine kupoteza maisha na mara ya pili ya matembezi hayo kuungwa mkono na Wamarekani wa rangi zote kutoka majimbo mengine huku yakiongozwa na Dr. Martin Luther King mwenyewe japo hawakuweza kuvuka lakini mauaji hayakutokea na kwa mara ya tatu pia yakiungwa mkono na Wamarekani wa rangi zote na huku yakiongozwa na Dr. Martin Luther King mwenyewe waliweza kufanya matembezi ya amani na kuvuka daraja hilo na Dr King kuhutubia mkutano wa historia uliowezesha kumshinikiza Rais wa Marekani wakati huo Lyndon B. Johnson kutangaza rasmi Wamarekani weusi kuanza kupiga kura. Matembezi hayo yataadhimishwa hapa Alabama kesho Jumamosi March 7, 2015 kwa Rais Barack Obama akiongozana yeye na mkewe na watoto kuwaongoza mamia ya wahudhuriaji katika kumbukumbu ya matembezi hayo.
Daraja la Edmud Pettus linalounganisha mji wa Selma na Montgomery
Daraja la Edmund Pettus katika picha

No comments: