Thursday, March 12, 2015

JUA HILI IRS SIKU ZOTE WAKIKUHITAJI HAWAPIGI SIMU, HUANDIKA BARUA

Kuna watu matapeli wamezuka hasa katika kipindi hiki cha kulipa kodi kwa IRS na timu ya Vijimambo imepata habari hii baada ya kuona kwenye kituo kimoja cha luninga kikielezea kuhusu utapeli huu na Vijimambo ikaona si vibaya kukumegea japo kidogo na wewe kama ulikua hufahamu uweze kuelewa kuhusu IRS wanapokua wanakutafuta hawapigi simu hukuandikia barua.

IRS wenyewe wanasema hua hawampigii mtu simu siku zote katika utendaji wao wa kazi humwandikia muhusika barua kama kama wanatatizo nae au kutaka ufafanuzi wa jambo fulani kutoka kwake kuhusiana na mahesabu yake ya ulipaji kodi.

IRS wameweka wazi kutokana na kutokea baadhi ya matapeli kujaribu kuwapigia simu watu na kuwataka walipe pesa kitu ambacho IRS wamekana kwamba wao hawampigii mtu simu siku zote wakikuhitaji watakuandikia barua.

No comments: