Thursday, March 12, 2015

KAMATI YA BUNGE YA MIUNDOMBINU ILIPOTEMBELEA OFISI ZA WAKALA WA MAJENGO TANZANIA (TBA)

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu Profesa Juma Athumani Kapuya akizungumza na watendaji wa Wakala wa Majengo nchini (TBA) kuhusu utekelezaji wa ujenzi wa nyumba za Serikali, wakati walipotembelea ofisi za Wakala jana jijini Dar es Salaam. Pembeni yake ni Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akieleza jambo kwa Kamati ya Bunge ya Miundombinu (hawapo pichani) kuhusuiana na mafanikio na changamoto zilizojitokeza katika utekelezaji wa miradi mbalimbali na hatua zilizochukuliwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA).
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Arch. Elius Mwakalinga akiongozana na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu, Prof. Juma Kapuya, wakati Kamati hiyo ilipotembelea nyumba za watumishi wa Serikali eneo la Ada Estate jijini Dar es Salaam.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Arch. Elius Mwakalinga akiwaongoza wajumbe Kamati ya Bunge ya Miundombinu kkwenda kukagua nyumba zinazojengwa kwa ajili ya watumishi wa Serikali eneo la Mabwepande, Dar es Salaam.
Kwa picha zaidi bofya soma zaidi
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu, Prof. Juma Kapuya akipewa ufafanuzi na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Arch. Elius Mwakalinga, wakati Kamati hiyo ilipotembelea nyumba za Serikali na kuona utekelezaji wake.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Arch. Elius Mwakalinga akiwaonesha baadhi ya nyumba ambazo zinajengwa na TBA (hazipo pichani)kwa ajili ya watumishi wa Serikali.
Baadhi ya nyumba za watumishi wa Serikali zinazojengwa na TBA eneo la Mabwepande.

No comments: