“Tumeuwona mkono wa Mungu, Tumeuona uwezo wake”
Tumaini Kilangwa: Mama, Mke, na Mjasiriamali |
Binafsi nakufahamu toka
mwaka 2003, ambapo wote tulikuwa tunaishi katika mji wa Wichita, Kansas
State. Lakini kuna wengi ambao hawakufahamu na wangependa kujua wewe ni
nani, na unafanya nini? Mimi naitwa Tumaini Kilangwa.
Nimezaliwa na kukulia Morogoro. Shule ya msingi nimesoma Mzumbe Primary
School. Masomo ya secondary nimesoma Msalato Secondary School kuanzia
Form one (I) hadi Form four (IV). Baada ya hapo nilienda Kilakala
Secondary School kwa Form Five (V) na Six (VI). Pia nime soma Advance
Diploma in Public Administration pale Mzumbe (IDM) / Mzumbe University,
ndipo baada ya hapo tukaja huku Marekani. Tunaishi Marekani toka mwaka
2000 mpaka sasa. Nimeolewa, nina watoto wawili, na kwasasa tunaishi
katika mji wa Wichita, Kansas mbapo nime jiajiri mimi mwenyewe katika
biashara ya mgahawa.
Tumaini, wewe kitaaluma una
bachelor degree ya Criminal Justice, na Masters ya Project Management;
nini haswa kilikufanya ukaacha kazi ya taaluma uliyo bobea nayo nakuamua
kufungua mgahawa ujulikanao kama Eastern Cuisines? Kuhusu
elimu na kazi nilizofanya dada Alpha; mimi nilisoma Tanzania chuo
kipindi hicho kilikuwa kinaitwa IDM-Insitute of Development and
Management, Mzumbe, ambayo sasa hivi imekuwa Mzumbe University.
Nakipindi kile tunasoma walikuwa wao hawajaanza kutoa degree kwahiyo
wote tuliosoma kipindi hicho tulipata Advance Diploma, hivyo nilisoma
pale na nikapata Advance Diploma in Public Administration. Nilipofika
hapa Wichita, Kansas nilisoma Certified Nurse Aide (CNA) nikafanya kazi
kama CNA kwa miaka miwili, nikaenda tena nikasoma Criminal Justice.
Baada ya kumaliza degree ya Criminal Justice nikafanya kazi na Mental
Health Association, na Sedgwick County Comcare.
Kusoma zaidi bonyeza HAPA
No comments:
Post a Comment