ANGALIA LIVE NEWS

Friday, March 27, 2015

Mkutano wa siku 4 wa Umoja wa vyama vya Walimu wa Nchi za Afrika Mashariki (FEATU)

Mratibu Msaidizi wa Utafiti na Mafunzo wa Umoja wa Vyama vya Walimu wa Nchi za Afrika Mashariki (FEATU) Bi. Lucy Njura Barimbui akiwasilisha mpango kazi wa miaka 5 ya Mtandao wa Wanawake wa Vyama vya Walimu wa Afrika Mashariki (WNEA) katika Mkutano wa siku 4 uliofanyika Hoteli ya Executive iliyopo Kilimani Mjini Zanzibar. 
Katibu Mkuu wa chama cha walimu Zanzibar (ZATU) Mussa Omar Tafurwa akichangia kitu katika Mkutano wa mpango kazi wa miaka 5 wa Mtandao wa wanawake wa Vyama vya walimu wa Afr. Mashariki.
Naibu Katibu Mkuu wa chama cha walimu Zanzibar (ZATU) Salim Ali Salim akifunga Mkutano wa siku 4 wa Umoja wa vyama vya Walimu wa Nchi za Afrika Mashariki (FEATU) uliofanyika Zanzibar
Baadhi ya washiriki wa Mkutano huo wakimba wimbo wa mshikamo mara baada ya kufungwa kwa Mkutano huo
Katibu Mkuu wa chama cha walimu Zanzibar Mussa Omar Tafurwa (wakatikati) katika picha ya pamoja ya wajumbe wa Mkutano wa Umoja wa vyama vya Walimu wa Nchi za Afrika Mashariki (FEATU). Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

No comments: