Mwalimu wa shule ya Sekondari Kibasila, Gaudensia Albert aliyekuwa akihifadhi kinyesi ndani kwake kwa miaka miwili amepelekwa Hospitali ya Muhimbili baada ya daktari wa Hospitali ya Temeke kubaini ana matatizo ya akili.
Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule hiyo, Kyando amesema baada ya kugundulika kwa tukio hilo walimpeleka Hospitali ya Temeke kwa kuangalia afya yake ambapo daktari akasema ana tatizo la akili, wakamuhamishia Muhimbili.
Baada ya kufikishwa Muhimbili madaktari walimpatia dawa ambazo anatumia mpaka sasa pamoja na ushauri.
“Sisi bado tunamhitaji kutokana na tatizo la uhaba wa walimu wa sayansi ulioko nchini”—alisema Mwalimu Kyando na kuongeza kuwa mbali na tatizo la kukutwa na kinyesi bado mwalimu huyo alikuwa anafundisha vizuri.
2 comments:
Mwalimu wa sayansi, labda alikua anataka kuzaliza umeme wake mwenyewe!!
Mwalimu huyu hana tatizo la akili.
Amevaa vizuri na vazi la heshima.
Ana afya njema. Haombi ombi chakula kwa watu wala hasumbui mtu. Anafundisha vizuri.
Anawahi kazini kila siku anaelewana na wanafunzi. Hajagombana na mtu.
Alihifadhi kinyesi chake ndani ya nyumba yake chumba kingine.
Mnapeleka Muhimbili kumpa dawa za nini? Akili yake ni timamu. Angalieni wale wanaokunya kenyesi barabarani na kukojoa mitaani mbona hamwapeleki Muhimbili?
Nyie ndio wasiona akili tamamu.
Mwachieni mwalimu wa watu akafundishe na aendele kufundisha.
Post a Comment