
Shoga, baada ya kusema hayo ngoja nirejee kwenye mada yangu ya leo inayohusiana na kuwafanyia masaji waume zetu kwa lengo la kuwaondoa uchovu na maumivu ya mwili.Nimeamua kutiririka na mada hii lengo likiwa lilelile la kuboresha uhusiano wa kimapenzi na waume zetu kwa sababu mambo ya mapenzi yana upana wake.
Nasema yana upana wake kwa sababu wapo wenzetu ambao suala la kuwafanyia masaji waume zao siyo geni na limekuwa ni utamaduni wao.Wapo ambao hawafanyi uzembe kabisa linapokuja suala la kuwakata kucha na nywele za sehemu mbalimbali waume zao na kuwaogesha kama watoto wadogo.
Ukiwaacha hao, wapo ambao wanapokuwa kwenye eneo la kujidai na waume zao, wanawadekea kadiri wawezavyo na wanapofurahishwa kima lovedave basi hulia mwanzo mwisho.Shoga, pamoja na kuelewa hayo yote leo nimeamua kuwapa darasa wenzetu ambao hawajui faida ya kuwafanyia masaji waume zao jambo ambalo ni muhimu sana kwa wanandoa.
Mtu asikudanganye shoga yangu, masaji kwa waume zetu ambao huwa bize na mihangaiko ya kutafuta shilingi ya kula watoto ina umuhimu sana na kuwafanya wanandoa kuwa karibu.Nasema kuwa karibu kwani baba anapomfanyia masaji mkewe halikadhalika na mke akafanya hivyo kwa ‘mista’ wake, huwa ni burudani ya aina yake.
Kwa kuelewa umuhimu wa masaji, kuna baadhi ya watu wamefungua sehemu maalum za kutoa huduma hiyo na wengi wanaokwenda huko ni wanaume.Shoga, hebu mpe raha mumeo kwa kumfanyia masaji ambayo haina gharama kwani ukiacha mafuta ya ‘wazungu’ unaweza kutengeneza mafuta ya nazi kisha ukamchua mumeo ambaye nakuapia kila atakapokuwa atakuwa akikuwaza wewe tu! Bye.
GPL
No comments:
Post a Comment